Friday, March 1, 2019

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI KISHAPU


2-6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wananchi waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Februari, 2019 amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo ametembelea mgodi wa Almasi wa Mwadui (Williamson Diamond Ltd) na kujionea shughuli za uchimbaji wa almasi pamoja na kupokea taarifa ya mgodi huo.
 Aidha alitembelea Shule ya Sekondari Shinyanga na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara, kuona mashine ya uchapaji wa maneno maalum kwa wasioona na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
 Akizungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo Makamu wa Rais amesema ziara yake hapo ilikuwa ya kuja kuwasalimu na kuona na kutambua changamoto zinazowakabili na kuwaahidi Serikali itazitatua na kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi na kuwataka walimu na wanafunzi wa kawaida kutowabagua au kuwaambia maneno ya maudhi wenzao wenye ulemavu.
 Makamu wa Rais ambaye ameongozana na Manaibu Waziri kutoka Wizara za Madini, TAMISEMI, Maji, Ujenzi, Kilimo na Ardhi kwa pamoja walitembelea mradi wa kituo cha Afya Kishapu ambao umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95% na umejengwa kwa fedha za Serikali shilingi milioni 400.
 Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mhunze, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa wilaya ya Kishapu kwa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ambapo pia mkoa unauhakika wa tani zaidi ya laki tano na ishirini elfu.
 Makamu wa Rais pia amekemea vitendo vya rushwa mkoani Shinyanga kwani kesi nyingi za mimba za utotoni zimeshindwa kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria kutokana na rushwa kutawala.
 Kwa upande wa Bima ya Afya, Makamu wa Rais ameukumbusha Uongozi wa mkoa huo na wilaya zake kuongeza juhudi za kuhamasisha wananchi kuwa na bima ya afya.
 “Kati ya Kaya 40,000 ni kaya 4000 tu zimechukua bima ya afya hapa Kishapu” alisema Makamu wa Rais.
3-3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wanafunzi waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
6-2
8-1
Meneja wa Huduma za Kiufundi wa Mgodi wa Williamson Diamond Richard Jumanne akimuonyesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan eneo ambalo uchimbaji wa almasi unafanyika katika mgodi huo uliopo Mwadui, Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
9-1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiangalia shughuli ya uchambuaji  wa almasi klatika mgodi wa Wiliamson Diamond Ltd, wengine pichani ni Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kulia). Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari  Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga mara baada ya kuweka  jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
15-2
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Shinyanga wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yup kwenye ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
16-1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Kishapu kwenye uwanja wa mikutano Mhunze mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
18-1 19-1

No comments :

Post a Comment