Mkuu wa Idara ya Maradhi ya Kina
mama na Uzazi Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt,Ummulkulthum Omar
akiwasilisha mada kuhusu Uzazi katika ufungaji wa Mkutano wa 11
wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Afya
waliohudhuria katika ufungaji wa Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya
Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
Mkurugenzi Utawala na Uwendeshaji
Hospitali ya Mnazi Mmoja Abubakar Khamis Hamad akiuliza maswali katika
mkutano wa 11 wakutathmini Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel
Zanzibar.
Daktari Bingwa wa maradhi ya akina
mama Hospitali ya Mnazi mmoja Hamed Mahfudh akifafanua baadhi ya
maswali yalioulizwa katika ufungaji wa Mkutano wa 11 wakutathmini Sekta
ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha
Ali Abdulla akitoa hotuba ya ufungaji wa Mkutano wa 11 wakutathmini
Sekta ya Afya katika ukumbi wa Verde Hotel Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na
Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na
Idara maalum za SMZ zitaendelea kujenga Nyumba za kuishi Wahudumu wa
afya katika kila eneo lenye Kituo cha Afya ili kuhakikisha wahudumu hao
wanapatikana muda wote hasa maeneo ya Vijijini.
Kwa kufanya hivyo kutapunguza kasi
ya wahudumu hao kukimbilia kufanyakazi Mijini na
kuviacha vituo vya
Afya vya Vijijini bila wahudumu.
Hayo yameelezwa katika Mkutano wa
11 wa kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya kwa mwaka 2017/2018 ikiwa ni
mapendekezo yaliyotolewa na washiriki wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi
wa Hotel ya VERDE, nje kidogo ya mjini Zanzibar.
Katibu wa Wizara ya Afya Asha Ali
Abdulla amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa kutokana na
kujadili mambo muhimu na mapendekezo ya kuimarisha huduma ya afya kwa
mwaka 2019/2020.
Amesema katika kukabiliana na
changamoto ya maradhi yasiyoambukiza ikiwemo Maradhi ya Miguu, Mgongo
ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi wengi wa Zanzibar Katibu huo
amesema mkutano umependekeza kufanya tafiti mbali mbali kubaini chanzo
cha maradhi hayo.
Hata hivyo amesisitiza kutolewa
kwa elimu ya afya kuhusu maradhi mbali mbali kama vile Shinikizo la
Damu, Kisukari na Saratani ili wananchi waweze kubadili mifumo yao ya
maisha ambayo huchangia ongezeko la maradhi hayo.
Amesema njia muhimu ni kuhakikisha
wananchi wanakula vyakula salama na kufanya mazoezi ya mara kwa mara
ili kuiepusha miili yao na kitisho cha maradhi hayo.
Kwa upande wake Atie Juma Shaame
Mkurugenzi wa Mipango sera na utafiti Wizara ya Afya amesema licha ya
huduma kutolewa bure Serikali itaendelea kuimarisha huduma hiyo kwa
kiwango cha juu kabisa.
Amesema kwa upande wa Serikali
kupitia Wizara ya Fedha imeahidia kushirikiana na Wizara hiyo pamoja na
washirika wa maendeleo ili kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata
huduma bora.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Baraza la Wauguzi Zanzibar Amina Abdulqadir amesema mkutano huo umekuwa
na mafanikio makubwa hasa kutokana na kushirikisha wadau wote kutoka
Serikalini na Taasisi binafsi ambao michango yao ilikuwa muhimu.
Amesema Sera ya ugatuzi itasaidia
kwa kiasi kikubwa kupatikana wauguzi watakaokidhi haja ya kila eneo na
kusisitiza serikali kutoa elimu kwa wananchi kufahamu maana halisi ya
ugatuzi.
“Ugatuzi kwa kweli umesaidia sana
kupeleka madaraka mikoani kubwa linalohitajika ni kuhakikisha kuwa
Wananchi wanapatiwa elimu wajue hasa maana ya Ugatuzi ili waweze kutoa
ushirikiano ipasavyo” alisema Mwenyekiti Amina
Amesema akiwa Mwenyekiti wa
Wauguzi jukumu lake ni pamoja na kuwakumbusha wenzake kutumia lugha
nzuri wakati wanapowahudumia wagonjwa.
kila inapofika kipindi cha
uandaaji wa Bajeti mpya Wizara ya Afya huwaita wadau wake wote kujadili
namna ya kuimarisha sketa hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kwa takriban miaka 15 sasa Wizara
ya afya imekuwa ikifanya mikutano ya kutathmini matokeo ya utekelezaji
wa kipindi cha mwaka mmoja ambapo mwaka huu mkutano huo wa siku mbili
umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 120 kutoka sekta binafsi, Washirika
wa maendeleo wakiwemo WHO, UNICEF, UNFPA, UNDP, ujumbe wa mwaka huu
‘‘Kuimarisha ushikiriano kwa lengo la kuinua huduma za Afya bora kwa
wote ’’
No comments :
Post a Comment