Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Julius Ndyamukama
wakwanza (kushoto) pamoja na Richard Mayongela watatu kutoka (kushoto)
ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere kukagua kazi ya upakaji wa rangi katika ndege aina ya Foker 50
iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali ambayo sasa itatumika
kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege aina ya Foker 50
iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba
abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Rais Dkt.
Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kazi
hiyo ambapo ingegharimu zaidi ya Shilingi milioni 160 wakati kazi hiyo
imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya shilingi miloni 7.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya ndani ya ndege hiyo
ambapo ufungaji wa viti vipya umekamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika ndege hiyo aina ya
Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa
itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wafanyakazi mbalimbali wa
Shirika la ndege la Air Tanzania hawapo pichani wakati akitoka kufanya
ukaguzi wa kazi ya upakaji rangi pamoja na uwekaji wa viti vipya katika
ndege hiyo aina ya Foker 50.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa ATCL
Ladislaus Matindi wakati wa Ukaguzi wa ndege hiyo aina ya Foker 50
Sehemu ya Ndani na nje ya Ndege
hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48
umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali
ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na
kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla
ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi
wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mafundi wazalendo
ambao wamefanya kazi ya kuandika na kuchora nembo ya Twiga pamoja na
kupaka rangi ndege hiyo ya Foker 50 kwa gharama ya Shilingi milioni 7.
Pia Rais Dkt. Magufuli amewazawadia mafundi hao kiasi cha Shilingi
milioni 10 kutokana na kazi yao nzuri ya kizalendo walioifanya. PICHA
NA IKULU
No comments :
Post a Comment