Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dk harrison Mwakyembe akizikiliza maelezo ya Meneja
NMB kanda ya Kusini Janeth Shango alipotembelea banda la benki hiyo
kabla ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji
mkoani Lindi.
Meneja Mwandamizi wa Biashara
ya Kilimo wa benki ya NMB, Carol Nyangaro akitoa mada baada ya ufunguzi
wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Lindi.
……………..
BENKI ya NMB imewahakikishia
wajasiriamali, wafanyabiashara na wakulima mkoani Lindi kuwa itaendelea
kuwahudumia kupitia huduma zake za kutunza fedha lakini pia kwa utoaji
wa mikopo.
Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kanda ya Kusini wa benki hiyo –
Janeth Shango, wakati
akizungumza kwenye jukwaa la fursa za biashara na
uwekezaji lilofanyika mkoani humo. Kama wadau wa sekta ya biashara
nchini, Benki ya NMB imedhamini wa jukwaa la Biashara linalofanyika
mkoani Lindi.
Jukwaa hilo lililoandaliwa na
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, liliwakutanisha washiriki takribani 350 wakiwemo
wawekezaji, wakulima, wajasiriamali, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali
na viongozi mbalimbali wa serikali.
Benki hiyo imefanya vizuri
katika sekta ya kilimo na kwa kutoa mikopo kulingana na mnyororo mzima
wa zao husika kupitia matawi yake 7, pamoja na kutoa huduma zingine za
kifedha kupitia mawakala zaidi ya 105 na mashine za kutolea fedha za ATM
mkoani humo.
Kwa upande wake, Meneja
Mwandamizi wa Biashara ya Kilimo wa benki hiyo Carol Nyangaro alisema
katika benki hiyo ambayo serikali ina hisa ya asilimia 30 kupitia bodi
ya mikopo iliidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya
mikopo ya wakulima na tayari shilingi bilioni 450 zimetumika.
NMB ni benki inayotambua kuwa
kilimo ndio uti wa mgongo nchini kwani asilimia 75 ya watanzania
wanajishughulisha na kilimo na hivyo itaendelea kuwekeza zaidi katika
kilimo.
No comments :
Post a Comment