Waziri wa Habari Sanaa
Utamaduni na Michezo Dr. Harison Mwakyembe (kulia) akimkabidhi bendera
Captain wa timu ya taifa ya riadha Marco Sylvester (kushoto) wakati wa
hafla ya kuiaga timu hiyo inayokwenda kushiriki mashindano ya dunia ya
mbio za nyika yanayofanyika nchini Denmark tarehe 30 mwezi huu. Tanzania
imepeleka timu ya wachezaji 16 na viongozi 4. Wafadhili wakuu wa timu
hiyo ni DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
……………………
- Yapeleka timu kubwa kuwahi kutokea katika historia
- Ufadhili wa DStv, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro watajwa kuwa sababu ya mafanikio
Timu ya Taifa ya riadha
itakayoshiriki mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika yatakayofanyika
nchini Denmark tarehe 30 Machi 2019, imeondoka nchini ikiwa na wachezaji
16 na viongozi 4 na kutajwa kuwa timu kubwa zaidi ya Tanzania kuwahi
kushiriki katika
mashindano hayo nje ya bara la Afrika. Timu hiyo
inajumuisha timu ya nyika ya wanaume (5), Timu ya Nyika ya wasichana (5)
na timu ya mchanganyiko ya mbio za kupokezana vijiti (Mixed relay)
Timu hiyo imeagwa na kukabidhiwa
bendera ya Taifa jana na waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo
Dr. Harison Mwakyembe katika hafla ambayo pia ilihudhuriwa na wafadhili
wakuu wa timu hiyo DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Waziri Mwakyembe ameikumbusha timu
hiyo kuwa wana jukumu kubwa sana la kupambana kufa na kupona ili kupata
medali na pia kuliletea taifa sifa. “Hivi karibuni tumeshuhudia
mafanikio makubwa katika michezo hapa nchini, tunatarajia kuwa
mtaliendeleza wimbi hili la mafanikio na ushindi kwa kuleta medali”
alisema waziri
Amewashukuru sana wafadhili wote
waliowezesha timu hiyo kwenda kuliwakilisha taifa hususan wafadhili
wakuu DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambao wamekuwa
wakidhamini riadha kwa muda sasa.
Mkuu wa uhusiano wa MultiChoice
Tanzania Johnson Mshana, amesema kuwa DStv wamekuwa wakidhamini riadha
kwa takriban miaka minne sasa na lengo la kubwa ni kuliandaa taifa kwa
ajili ya mashindano makubwa duniani ya Olyimpic yatakayofanyika Tokyo
Japan mwaka 2020.
“Tuna mkakati wa kuliandaa taifa
kushiriki na kushinda katika Olyimpic. Dhamira yetu kuona wimbo wetu wa
taifa unapigwa kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo makubwa. Lakini
hili haliwezi kutokea ikiwa hatutawekeza nguvu kubwa mapema”
alisisitiza Mshana
Naye Mkuu wa Uhusiano wa Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro Joyce Mgaya, amesema Mamalaka hiyo imeamua
kuwekeza kwenye riadha kwani ni sehemu muhimu ya kulitangaza taifa letu
na hivyo fursa kubwa ya kukuza utalii ambayo ni sekta muhimu sana katika
ukuaji wa uchumi wa nchi.
“Kwa kuwa na timu na wachezaji
wanaofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, tunaweza kuitangaza
nchi yetu kote ulimwenguni kirahisi zaidi na hivyo kuchangia sana katika
kukuza utalii wetu na hii ndiyo dhamira kubwa ya Mamlaka yetu.
Tunaamini timu yetu hii, kuw ukubwa na ubora wake itafanya vizuri kwenye
mashindano haya ya Dunia”.
Timu hiyo ilichaguliwa baada ya
mashindano ya Taifa ya mbio za nyika yaliyofanyika mjini Moshi Februari
mwaka huu na inatarajiwa kurujea nyumbani tarehe 31 Machi 2019
No comments :
Post a Comment