MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA
AMEFANYA UTEUZI NA KUWAPANDISHA VYEO BAADHI YA MAOFISA WA POLISI KUWA
MAKAMISHNA WA POLISI NA KUWAHAMISHA WENGINE WAWILI KAMA IFUATAVYO;
……………………………………………………………
- NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) CHARLES MKUMBO AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI INTELIJENSIA YA JINAI (CP INTEL)
- NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) LIBERATUS MATERU SABAS AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI OPERESHENI NA MAFUNZO (CPO&T)
- NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) SHABAN MLAI HIKI AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI MAABARA YA UCHUNGUZI WA KISAYANSI (CP F&B)
- NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) LEONARD PAUL LWABUZALA, AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYONGOZA KAMISHENI YA POLISI FEDHA NA LOJISTIKI (CPF&L)
- KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI SACP BENEDICT MICHAEL WAKULYAMBA, AMETEULIWA NA KUPANDISHWA CHEO NA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA KAMISHNA WA POLISI, ATAKAYEONGOZA KAMISHENI YA POLISI UTAWALA NA MENEJIMENTI YA UTUMISHI (CPA&HRM)
WALIOHAMISHWA KWENDA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI NI WAFUATAO:
- KAMISHNA ALBERT MATHIAS NYAMHANGA, KUTOKA KAMISHNA WA POLISI UTAWALA NA MENEJIMENT YA UTUMISHI KWENDA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA WAKIMBIZI.
- KAMISHNA NSATO MSSANZYA MARIJANI, KUTOKA KAMISHNA WA POLISI OPERESHENI NA MAFUNZO KWENDA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA WAKIMBIZI.
WAKATI HUO HUO, INSPEKTA JENERALI WA POLISI AMEFANYA UHAMISHO WA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA, KAMA IFUATAVYO:
- KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI GEMINI S. MUSHI, ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA RUVUMA KWENDA KUWA MKUFUNZI MKUU CHUO CHA POLISI (CCP) MOSHI
- KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI (SACP) RENATA M. MZINGA, ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA NJOMBE ANAKWENDA MAKAO MAKUU YA POLISI DSM
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) SIMON SILVERIUS HAULE, ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA SHINYANGA ANAKWENDA MAKAO MAKUU POLISI DSM
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) JONATHAN SHANA, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA ARUSHA
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) AMON DAUD KAKWALE, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA KIPOLISI TEMEKE
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) SIMON MARWA MAIGWA, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA RPC RUVUMA
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) SALUM RASHID HAMDUNI, ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA NJOMBE
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) RICHARD GEORGE ABWAO ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI (RPC) MKOA WA SHINYANGA
- KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) ZUBER SEIF CHEMBERA ANAKWENDA KUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIPOLISI ILALA.
MAKAMISHNA WALIOTEULIWA NA MHE.
RAIS WATAAPISHWA NA INSPEKTA JENERALI WA POLISI KWA NIABA YA MHE. RAIS
TAREHE ITAKAYOPANGWA, MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI.
Imetolewa na:
Simon N. Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
No comments :
Post a Comment