Friday, March 1, 2019

RC Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti: Mwili wa Ruge Mutahaba kuagwa katika Viwanja vya Gyhmkana mjini Bukoba


index
Mkuu wa Mkoa Kagera,  Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti na baadhi ya wanakamati wa maandalizi ya mazishi ya Ruge Mutahaba mkoani Kagera.
Na Mwandishi wa Fullshangwe Bukoba
Mkuu wa Mkoa Kagera,  Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amesema. Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba unatarajiwa kuagwa Katika viwanja vya Gyhmkana ndani ya Manispaa ya Bukoba Kabla ya kupelekwa Kabale Halmashauri ya Wilaya Bukoba, kwa ajili ya Ibada na Mazishi hii ni kutokana na Wingi wa watu na sehemu ya Nyumbani kuwa Finyu.
Aidha kwa upande mwingine Mh. Gaguti amewaomba wananchi kujitokeza kuulaki mwili wa Marehemu Ruge popote pale utakapopita kwa ajili ya kutoa salaam za mwisho ikiwa ni Ishara ya kumuenzi na kumuaga Mzalendo na mwanaharakati wa kweli  Marehemu Ruge Mutahaba

No comments :

Post a Comment