Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi
akizungumza na Waandishi wa habari Kabla ya kutiliana Saini na Miss
Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune katika Ofisi za TTB Zilizopo
Jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kutiliana Saini Mkataba wa kuwa Balozi wa Bodi ya Utalii Nchini.
Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi wakitiliana saini Mkataba wa mrebo huyo kuwa balozi wa utalii nchini
Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi, Wakibadilishana Mkataba mara baada ya kuliana Saini
Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika kushuhudia utiliaji saini Mkataba wa Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Mukune amesaini mkataba
wa kuwa Balozi wa Bodi ya Utalii Tanzania leo March28 2019 kwa kutangaza Utalii wa ndani na kutoa hamasa kwa watanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya
utiaji saini mkataba huo wa mwaka mmoja Queen Elizabeth anasema kuwa
yeye anaona fahari kubwa kupata nafasi ya kuwa balozi wa kutangaza
vivutio vyetu hivyo amefurahi kupata nafasi hiyo.
“nimefurahi
kupata nafasi ya kutangaza vivutio vyetu ndani na nje ya nchi na
naahidi kuitumia nafasi hii vizuri kabisa kwa kutumia nafasi na
umaharufu wangu nilionao kwa sasa kwa kuwa mfano wa Mrembo ambaye
nitafanya ziara ya utalii wa ndani kama taji langu linavyojieleza kwani
nitatoa hamasa kupitia mitandao yangu ya kijamii na makundi yote
yanayoniunga mkono hili waweze kutembelea vivutio vyetu vilivyopo hapa
nchini”anasema
Naye
Mkurugenzi Mwendeshaji wa bodi ya Utalii nchini Devotha Mdachi anasema
katika kuendelea kutangaza utalii wa nchi wamehamua kutumia vijana wenye
ushawishi ili kuzidi kuitangaza utalii wetu kwa watanzania na wageni
wanaotuzunguka.
“Tumeamua
kumtumia Miss Tanzania kwanza ni kijana pia anaushawishi mkubwa kwa
jamii kwa watu wengi kwani ameweza kutuwakilisha kimataifa hivyo kupitia
yeye tutaweza kutangaza vivutio vyetu vikafika mbali na kuwafikia
vijana wengi hapa nchini ambao wamekuwa wakifatilia masuala ya burudani
na urembo”anasema.
anasema wataendelea kuwatumia vijana maarufu kuzidi kutangaza utalii wa nchi na wameshaanza mazungumzo na baadhi yao.
No comments :
Post a Comment