Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amekutana na
kufanya mkutano na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Guastavo
Rodriguez Roller. Mkutano huo ulijikita katika kuwajengea uwezo wakulima
kwenye mazao ya kimkakati, ikiwemo kilimo cha pamba, miwa na maembe.
Mkutano ukiendelea kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wa Cuba ukioongozwa na Mhe. Guastavo Rodriguez Roller. |
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali
ya Cuba kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo kwa mtazamo wake wa
kuanzisha ushirikiano mpana zaidi baina ya Zanzibar na Tanzania katika
sekta hiyo muhimu.
Akizungumza
na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller,
katika makao makuu ya wizara hiyo mjini Havana, Balozi Seif alieleza
kuwa, Zanzibar na Cuba zimekuwa na ushirikiano ya karibu katika sekta za
afya na elimu kwa kipindi kirefu sasa suala ambalo limeleta mafanikio
makubwa.
Balozi
Seif alibainisha kuwa, kwa kuwa maonyesho ni moja ya njia ya
kubadilishana mawazo kitaaluma alimuomba Waziri wa Kilimo wa Cuba
kutenga muda wa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya
Tanzania yanayofanyika mwezi Agosti wa kila mwaka nchini.
Kwa
upande wake, Mhe. Roller alibainisha kwamba, Cuba imebarikiwa kuwa na
hekta milioni 10,000,000 ambazo zinatoa ajira kwa wakulima zaidi ya
5,000.Alifafanua kuwa, asilimia
70% ya ardhi hiyo ina maliasili, asilimia 3.5 inatumika kufuga na zaidi
ya asilimia 60 inatumika katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na
kilimo pekee.
No comments :
Post a Comment