Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi, ametembelea shamba la mimea asilia ( organic farm ) nchini Cuba, ambapo alipata maelezo juu ya uzalishaji wa mazao mbalimbali bila kutumia kemikali ambapo mradi huo umeweza kuajiri wafanyakazi takribani 200 wakiwemo wazee na vijana. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shamba hilo, wa pili kutoka kulia ni mkalimani Bi. Beatriz Soto na wa kwanza kushoto ni Afisa kilimo, Bw. Jose Antonio.
Mhe. Dkt. Ussi akiendelea kupata maelezo juu ya kilimo cha miwa. |
Juu na chini Mhe. Dkt. Ussi akipata maelezo namna ya utengenezaji wa mbolea isiyokuwa na kemikali yeyote. |
Bw. Lopezi akimwonyesha Mhe.Dkt. Ussi teknolojia ya kifaa cha kupandia mazao. |
Mhe. Dkt. Ussi akizungumza na mmoja wa wakulima kwenye shamba hilo, aliyeonekana kufurahishwa na ujio wa Watanzania. |
Sehemu ya mazao yanayopatikana kwenye shamba hilo. |
No comments :
Post a Comment