Makamu
Mwenyekiti wa Bodi hiyo balozi James Nzagi akizungumza jambo mbele ya
wajumbe wenzake na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Katavi.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO wakishuka katika moja ya
mashine ya kufua umeme. Aliyeko mbele ni meneja wa TANESCO mkoa wa
Katavi Felix Olang’
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wakikagua Mita za kupima matumizi ya
umeme. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo balozi James Nzagi
Wafanyakazi
wa TANESCO mkoa wa Katavi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika hilo alipofanya ziara mkoani Katavi leo
Wafanyakazi
wa TANESCO mkoa wa Katavi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika hilo alipofanya ziara mkoani Katavi leo
Baadhi ya matenki ya mafuta yanayotumika kuendesha mitambo hiyo ya kufua umeme mkoani Katavi.
Mitambo ya kufua umeme iliyopo mjii Mpanda mkoani Katavi.
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Katavi
Bodi
Ya Wakurugenzi Ya Shirika La Umeme Nchini (Tanesco) Imefanya Ziara Ya
Siku Moja Mkoani Katavi Kwa Lengo La Kukagua Mashine Za Kuzalishia Umeme
Pamoja Na Kutambua Changamoto Mbalimbali Zinazohusiana Na Utoaji Wa
Huduma Ya Nishati Ya Umeme Katika Mkoa Huo
Akizungumza
Na Wafanyakazi Wa Tanesco Mkoa Wa Katavi; Makamu Mwenyekiti Wa Bodi Ya
Wakurugenzi Ya Tanesco Balozi James Nzagi Amewataka Wafanyakazi Kujituma
Kufanya Kazi Kwa Bidii Na Kupata
Wateja Wa Kutosha
Ameongeza Kuwa Dhamira Ya Shirika Ni Kuwa Na Zaidi Ya Megawati 5000 Hali Itakayowezesha Uendeshaji Wa Tanzania Ya Viwanda
Kwa
Upande Wake Meneja Wa Tanesco Mkoa Wa Katavi Bwana Felix Olang Amesema
Kwa Sasa Shirika Limeshindwa Kuunganisha Zaidi Ya Wateja 15,000 Kutokana
Na Kuwa Na Mashine Chache Za Kufua Umeme
Ametaja
Mashine Hizo Kuwa Tatu Ziko Katika Manispaa Ya Mpanda Na Zina Uwezo Wa
Kuzalisha Megawati 3.7 Na Moja Iko Inyonga Wilaya Mlele Yenye Uwezo Wa
Kuzalisha Umeme Kilowati 420
Bwana
Olang’ Amesema Hali Hiyo Imepelekea Kuwa Na Mteja Mkubwa Mmoja Tu
Ambaye Ni Mamlaka Ya Maji Safi Na Maji Taka (Muwasa); Huku Wakishindwa
Kuunganisha Wateja Walio Katika Migodi Ya Madini mbalimbali Ya Dhahabu
Na Madini Ya Ujenzi
Pia
Ameiomba Bodi Kuangalia Katavi Kwa Jicho La Pekee Kuiongezea Mashine
Pale Zinapopatikana Kwani Katika Mikoa Mingine Kuna Mashine Za Ziada
Awali
Mjumbe Wa Bodi Hiyo Bwana David Alal Amesema Baadhi Ya Mikoa Ambayo
Haijaunganishwa Na Umeme Wa Gridi Ya Taifa Inakabiliana Na Changamoto
Mbalimbali Za Uendeshaji Wa Vituo Vya Uzalishaji Umeme
Amesema
Licha Ya Changamoto Hizo Watumishi Wa Shirika Hilo Wanapaswa Kuwa
Mstari Wa Mbele Katika Kuhudumia Wateja Na Kukwepa Kashfa Kama Za Lugha
Chafu Na Rushwa Ili Kuwezesha Shirika Kufanikiwa Kujitegemea
“Tukiwahudumia Vizuri Tutaongeza Wateja, Tukiongeza Wateja Mapato Yataongezeka” Alisema Alal.
No comments :
Post a Comment