Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea nyaraka kutoka kwa Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba
Kabudi wakati alipomkabidhi rasmi ofisi baada ya kubadilishana wizara
hizo kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa hivi
karibuni na Mhe. Rais. Makabidhiano hayo yamefanyika makao maku ya
Wizara yaliyo katika Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM- jijini Dodoma,
wakiangalia kushoto kwa prof Kabudi ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju
na kulia ni Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Mkurugenzi wa Mashtaka
Bw. Biswalo Mganga na watumishi wengine wa Wizara
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akishikana
mkono na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga
baada ya kumkabidhi ofisi rasmi baada ya kubadilishana wizara hizo
kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa hivi
karibuni na Mhe. Rais. Makabidhiano hayo yamefanyika makao maku ya
Wizara yaliyo katika Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM-
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga (watatu kulia) katika picha ya pamoja na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi (wanne kulia) baada ya kutembelea jengo la Wizara ya
Katiba na Sheria lililoko katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma
ambako pia alitumia nafasi hiyo kumkabaidhi jengo hilo kama asehemu ya
makabidhiano ya Wizara baina ya Mawaziri hao.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akitia
saini kitabu wa cha wageni baada ya kukagua jengo la Wizara ya Katiba na
Sheria na kulikabidhi jengo hilo kwa Waziri wa sasa wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (mwenye tai ya Bluu) anayeongea na
Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome. Jengo hilo liko katika mji wa Serikali
Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi
wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Agnela Chang’a baada ya kuwasili katika
ofisi za Wizara jijini Dodoma tangu apishwe kushika nafasi hiyo , huku
aliyekuwa Waziri Mhe, Prof. Kabudi na Katibu Mkuu Prof. Mchome
wakiangalia.
Waziri wa Katiba na Sheria mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiambatana na Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof.Palamagamba Kabudi (nyuma
yake) na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome
wakisalimiana na watumishi wa Wizara baada ya kuwasili makao makuu ya
Wizara UDOM kwa ajili ya kukabidhiana Ofisi baina ya Mawaziri hao
kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Mhe.
Rais hivi karibuni.
Waziri wa Katiba na Sheria mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiambatana na Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki mhe. Prof.Palamagamba Kabudi (nyuma
yake) wakisalimiana na watumishi wa Wizara baada ya kuwasili makao makuu
ya Wizara UDOM kwa ajili ya kukabidhiana Ofisi baina ya Mawaziri hao
kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Mhe.
Rais hivi karibuni.
………………………..
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewasili makao makuu ya Wizara jijini
Dodoma na kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. Kitendo hicho kinafuatia kubadilishana
wizara baina ya mawaziri hao kufuatia mabadiliko madogo katika Baraza la
Mawaziri yaliyofanywa na Mhe. Rais DKt. John Pombe Magufuli Machi tatu
mwaka huu.
Akikabidhi ofisi Prof. Kabudi
amewashukuru watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kwa
ushirikiano
waliompatia katika kipindi alichofanya nao kazi na kuwasihi kuendelea
kumpa ushirikiano kama huo Balozi Dkt. Mahiga kwani anaamini yale
aliyoyaanzisha yataendelezwa na Waziri huyo kwa nguvu zote.
Prof. Kabudi amesema katika
kipindi chake cha uongozi Wizarani amebadilisha muundo wa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali nakutoa ofisi mpya tatu za Mwanasheria Mkuu
wa Serikal, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa
Serikali na ana imani kuwa mabadiliko hayo yatatekelezwa kikamilifu
chini ya uongozi wa mjenzi mahiri Dkt. Augustine Mahiga.
“Mlinipa ushirikiano mkubwa katika
kipindi change, niwasihi muendelee hivyo kwani kwa kushirikiana nanyi
tulifanikiwa kubadilisha muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na hivyo kutoa ofisi mpya tatu za Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, natumai
kuwa utekelezaji wa majukumu yaliyo mbele yao utakuwa kamilifu chini ya
Mhe. Balozi Dkt. Mahiga ambaye ni mjenzi Mahiri kama mtashirikiana
vyema,” alisema Prof. Kabudi.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa
Ofisi Mhe. Balozi Dkt. Mahiga amesema amepokea jukumu hilo kwa mikono
miwili na amewashukuru watumishi wa Wizara hiyo kwa mapokezi waliompatia
na kuahidi kushirikiana na watumishi wote katika kazi zao na hivyo
kuendeleza yale yote ambayo Prof. Kabudi ameyaacha kwa ajili ya kuiletea
nchi maendeleo kupitia sekta ya Sheria nchini.
“Niwashukuru kwa mapokezi yenu leo
hii, nimefarijika kuwa nanyi hapa siku hii kama ambavyo Mhe. Rais
alisema siku naapishwa kuwa nisiwe na shaka nimezungukwa na wanasheria
mahiri, niwaahidi kuwa tutashirikiana katika kazi zote ili tuendeleze
yale yote ambayo mwanafunzi wangu Prof. Kabudi ameishia,” alisema Balozi
Dkt. Mahiga
Awali mawaziri hao walikabidhiana
majengo ya ofisi zao yaliyoko katika Mji wa Serikali Mtumba na baadaye
kuja zilizoko Ofisi za Wizara zilizoko Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM
ambako walikabidhiana taarifa mbalimbali za Wizara na kuzungumza na
watumishi.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na
katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria prof. Sifuni Mchome, Naibu
Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga
na watendaji wengine wa Wizara na taasisi zake waliopo Jijini Dodoma.
No comments :
Post a Comment