Mwakilishi wa benki ABC Bw.
Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa
mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
Mwakilishi wa benki ABC Bw.
Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah
Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi
msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)
Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya
Kilindi Bi. Sauda Mtondoo akizungumza na watu mbalimbali na kutoa
shukurani za dhati kwa BancAbc kwa kuwapatia msaada wa mabati 200,
katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za manispaa ya Kilindi
mkoani Tanga.
Mheshimiwa Sauda Salum
Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati yaliyotolewa na
BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.
Mwakilishi wa benki ABC Bw.
Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akipeana mkono na mkuu
wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo baada ya kukabidhi msaada wa
mabati 200. Wengine katika picha ni Asmah Abubakar na Raphael Kalinga wa
BancAbc
Mwakilishi wa benki ABC Bw.
Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah
Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa
mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
……………………………….
BancABC kupitia Huduma yetu ya
Mkopo Rahisi imejidhatiti kuweza kuhakikisha kwamba
tunainua kuendeleza
mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hii inafanya shughuli zake
kupitia miradi yetu ya kusaidia jamii inayotuzunguka.
Sisi BancABC tunaamini kwenye
umuhimu wa elimu bora katika jamii zetu hapa Tanzania na kwa hivyo
tunaunga mkono Serikali ya Awamu ya 5 na hususani Rais wetu Mhe. John
Pombe Mafuguli Katika miradi mbali mbali ya elimu kwa lengo la kuinua
kiwango cha elimu na kuweza kuwafikia kila jamii na hasa maeneo ya
vijijini kwa wale ambao wako kwenye hali duni.
Akizungumza katika hafla hiyo
fupi Bw. Emmanuel Nzutu ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi
alisema; “Kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa
kila Mtanzania kuanzia chekechekea hadi kidato cha nne, Leo Bancabc
tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu
tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo.”
Napenda kuchukua fursa hii
kuwakaribisha Bancabc na pia kuwajulisha kuwa benki yetu tunatoa huduma
ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans
ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile
vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa
ule wa awali.
Uzuri wa mkopo huu tofauti na
mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo anaweza kuchagua ni mradi
gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa karo ya shule, kununua
gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi ya nyumba au kumalizia
ujenzi.
Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya.
‘Mkopo huu utakuwa na bima ya
maisha pale ambapo mwenye Mkopo anapofariki, familia yake inapewa pesa
taslimu Tzs500, 000 kwa ajili ya kugharamia mazishi.’
Tunatoa wito kwa wateja wetu na
wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia
Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto zako.
No comments :
Post a Comment