Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa
Umma, Bi. Immaculate Ngwale alipowasili Ofisi za Tume ya Utumishi wa
Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam kuzungumza na watumishi wa Tume
hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa
Umma, Jaji Mstaafu Dkt. Stephen Bwana akimkaribisha Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa Tume
wakati wa kikao kazi kilichofanyika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma,
Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Katibu, Tume ya
Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo.
Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa
Umma, Bw. Richard Odongo akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao kazi
kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na
watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Ofisi za Tume ya
Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi kati yake
na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume
ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu, Dkt. Stephen Bwana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst)
George Mkuchika (Mb) akizungumza na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa
Umma kabla ya kuanza kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya
Utumishi wa Umma, Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini
Dar es Salaam.
Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa
Umma, Bi. Rosy Elipenda akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watumishi
wa Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi
wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza
jijini Dar es Salaam.
……………………………
Watendaji katika Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka, Sekretarieti za mikoa na
Halmashauri
za wilaya nchini wametakiwa kutokwamisha jitihada za Tume ya Utumishi wa
Umma katika kushughulikia rufaa za mashauri ya watumishi wa umma kwa
kutuma vielelezo sahihi vinavyohitajika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mkuchika amesema kuwa, baadhi
ya waajiri na watumishi wa umma wamekuwa wakikaidi au kuchelewa
kutekeleza maelekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma ya kuwataka kuwasilisha
vielelezo vinavyowezesha ushughulikiaji wa rufaa za mashauri ya
watumishi jambo linalokwamisha ushughulikiaji wa rufaa za watumishi.
Amewataka waajiri na watumishi wa
umma nchini kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tume ya Utumishi wa Umma kila
wanapotakiwa kufanya hivyo na kumwagiza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi
wa Umma kuorodhesha waajiri wote watakaoendelea kukaidi maagizo ya Tume
ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.
Mhe. Mkuchika
amewatahadharisha watumishi na waajiri wanaokwamisha michakato ya
ushughulikiaji wa rufaa za watumishi kuwa wanaathiri dhana nzima ya
utawala bora na wanakwamisha utoaji wa haki kwa watumishi wa umma na
kusisitiza kuwa hatomvumilia mwajiri au mtumishi yeyote anayeharibu
heshima yake aliyoijenga kwa miaka mingi.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi
wa Tume ya Utumishi wa Umma, Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma Bi.
Rosy Elipenda amemhakikishia Waziri Mkuchika kuyafanyia kazi maelekezo
yote aliyoyatoa na kuongeza kuwa Tume itaendelea kutekeleza majukumu
yake kwa weledi na uadilifu bila upendeleo wowote.
No comments :
Post a Comment