Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati alipotembelea Benki ya Biashara ya DCB tawi la
Dodoma leo
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
Biashara ya DCB Bw.Godfrey Ndalahwa(katikati) akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo,wakati
alipotembelea Benki ya Biashara ya DCB tawi la Dodoma leo
Baadhi ya waandishi wa habari
pamoja na wafanyakazi wa benki ya DCB wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati alipotembelea Benki ya Biashara ya
DCB tawi la Dodoma leo
Mteja wa Benki ya DCB akipata huduma katika tawi lililopo jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya DCB
alipotembelea leo katika tawi hilo lililopo jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa Benki ya DCB Tawi la Dodoma
leo alipofanya ziara ya kujionea shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
…………………….
Na. Majid Abdulkarim
Benki ya Biashara ya DCB iliyoka
chini ya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), imetakiwa kuwajengea uwezo mzuri wateja wao katika
kufanyikisha mahitaji yao ya ujasilia mali ili kuweza kupata matokeo
chanya na kupata kipato kizuri
kitakacho wasaidia kuinua uchumi wa Nchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo wakati alipotembelea Benki ya Biashara ya DCB tawi la
Dodoma leo jijini Dodoma.
Mhe.Jafo ameutaka uongozi wa Benk
ya DCB kuwapatia elimu watejeja wao juu ya kufanya ujasilia mali au
biashara zao kwa kuwaongoza namna gani wataweza kufikia malengo yao
katika shughuli wanazo fanya ili kuhakikisha wanafikia malengo yao kwa
ufasaa.
Aidha Jafo amesema kuwa sasa ni
wakati wa DCB benki kujenga ushirikiano mzuri na uongozi wa jiji la
Dodoma na wao kuwa na hisa katika benki hiyo kwani jiji la Dodoma ni
miongoni mwa majiji kumi yanayofanya vyema katika ukusanyaji wa mapato
hapa nchini .
“Natoa wito kwenu kuwa mnatakiwa
kuwa na ukarimu kwa wateja wenu ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi
ya haya, kwani lugha nzuri utakayo tumia katika kumuhudumia mteja wako
ndo itakayo mfanya mteja kufurahiya huduma yako na kupata wateja wengi
zaidi ya hawa mlonao kwa sasa”Ameongezea Mhe. Jafo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
Biashara ya DCB Bw.Godfrey Ndalahwa amesema kuwa mpka sasa uboreshaji wa
huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio chachu ya kumuwezesha mteja
kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenk, kutunza pesa na
kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Bw. Ndalahwa ameongezea kuwa benki
inamalengo ya kujitanua zaidi tofauti na awali ilikuwa benki ya Jumuiya
ya Wananchi wa Dar es salaam na kwa sasa malengo ni kujitanuaa katika
halmashauri, manispaa na majiji ya nchi nzima.
“Benki hii ilianzishwa mnamo mwaka
2001 ikiwa kama benki ya wananchi wa Dar es salaam , Rais wa Awamu yta
Tatu , munamo 2001, alitoa agizo la kuanzisha benki hii na ikiwa kama
benki ya Jumuiya ya Wanachi kupitia Manispaa za Jiji la Dar es salaam
ikiwemo Halmashauri ya Jiji” Amehitimisha Bw. Ndalahwa.
No comments :
Post a Comment