Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza nafasi za
ajira kwa Walimu 4,549 wa Shule za Msingi na Serkondari katika mwaka wa
fedha 2018/19 leo jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imetangaza nafasi za
ajira 4,549 za walimu wa shule za msingi na sekondari katika mwaka wa
fedha 2018/19 ili kupunguza uhaba wa walimu ulipo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,amesema
Serikali inajua kuwa kuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu
nchini hasa uhaba wa walimu hivyo itaajiri walimu ili kupunguza uhaba
uliopo.
Hata hivyo Jafo amesema kuwa
ajira hizo mpya kwa waombaji zinapaswa kuomba kwa njia ya mtandao na
mwisho wa kupokea maombi utakuwa Machi 15, mwaka huu.
”Serikali ya awamu ya tano chini
ya Rais John Magufuli inaendelea kuongeza idadi ya watumishi katika
sekta ya umma kwa kutoa nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana wa
kitanzania katika sekta ya Elimu”amesema Jafo
Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi
ya Rais Tamisemi inawatangazia walimu wenye sifa hizo kutuma maombi yao
kwa njia ya mtandao (Online Teacher Employment Application
System-OTEAS).
Jafo amesema kuwa kwa walimu wa
shule za msingi wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma
Daraja la IIIA wenye Astashahada ya ualimu, na wenye daraja la IIIB
wenye Stashada (Diploma ya ualimu katika masomo ya Kingereza, Uraia,
Historia, Jiografia na kiswahili.
Aliongeza kuwa walimu wenye
sifa ya Daraja la IIIC wenye shahada ya ualimu kwa masomo ya
Kingereza,Uraia,somo la ziada,Historia,Geographia na Kiswahili.
Jafo ametangaza kundi jingine
lenye sifa ni Mwalimu mwenye Daraja la IIIC na mwenye mahitaji maalum
aliyehitimu Shahada kwa masomo ya English,Uraia,somo la
ziada,Historia,Geographia na kiswahili.
Kwa walimu wa sekondari Waziri
Jafo amesema kuwa wao wanaotakiwa kufanya maombi ni Mwalimu wenye
Daraja la IIIC mwenye Shahada ya ualimu aliyesomea Elimu maalum.
Jafo amesema wengine ni wenye
Daraja la IIIB wenye Stashahada (Diploma) ya ualimu waliosomea Elimu
maalum na mwalimu Daraja la IIIB mwenye Stashahada ya ualimu somo la
Mathematics, Biology, Physics,na Chemistry.
Amesema wengine wenye sifa za
kuomba ni mwalimu daraja la IIIC mwenye shahada ya ualimu somo la
Agriculture Science, na mwalimu wa Daraja la IIIC mwenye Shahada ya
ualimu somo la Home Economics na mwalimu Daraja IIIC mwenye Shahada ya
ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry na Biology.
Aidha Jafo ameongeza kuwa
walimu wengine ni wa Daraja IIIC wenye shahada ya ualimu somo la Book
keeping, Commerce, Accounts na Economics na mwalimu daraja la IIIC
mwenye Shahada ya ualimu somo la English, Civics na General Studies.
Hata hivyo Jafo amesisitiza kuwa
waombaji wenye sifa zote hizo wanatakiwa kuwa watanzania, wawe
wamehitimu kati ya mwaka 2014 hadi 2017 isipokuwa kwa kundi maalum la
wahitimu wa elimu ya ualaimu wa masomo ya Fizikia na Hisabati.
Jafo amesema kuwa sifa nyingine
ya jumla kwa muombaji asiwe na umri zaidi ya miaka 45, na wakati wa
kutuma maombi walimu ambao waliwahi kutuma na hawajaajiriwa wanapaswa
kutuma upya.
No comments :
Post a Comment