Meneja
Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akitangaza rasmi
promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja
akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile
alicholipia. Promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili
itaishia mwisho wa mwezi wan ne.
Meneja Masoko
wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akielezea promosheni maalum ya
kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha
juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia.
Promosheni hiyo itaanza inaanza rasmi tarehe 1 Machi na itaendelea kwa
muda wa miezi miwili. Kulia ni Meneja Uhusiano Johnson Mshana na
katikati ni Meneja Uendeshaji Ronald Shelukindo
Meneja Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania Johnson Mshana akieleza kuhusu promosheni maalum ya
kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha
juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia.
Promosheni hiyo itaanza inaanza rasmi tarehe 1 Machi na itaendelea kwa
muda wa miezi miwili
………………………………………………………………………………….
Kampuni ya MultiChoice Tanzania
kupitia huduma zake za DStv imetangaza tena ofa mpya na kabambe kwa
wateja wake inayojulikana kwa jina la “Step Up” ambapo mteja wa DStv
atatakiwa kufanya malipo ya mwezi ya kifurushi cha juu ya kile
anachotumia na kisha
kupatiwa kifurushi cha juu zaidi ya kile
alicholipia kwa kipindi cha mwezi mzima bila malipo ya nyongeza.
Akizungumza wakati wa kutangaza
ofa hiyo Meneja Uendeshaji wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Ronald
Shelukindo alieleza kuwa Ofa ya‘Step Up’ ni kampeni maalum kwa
wateja wa DStv yenye lengo la kuwatunuku wateja wanaolipia kifurushi cha
juu ya kile anachotumia. Wateja wa vifurushi vya Bomba, Family na
Compact watakaolipia kifurushi kinachofuatia juu yake watatunukiwa
kufurushi cha juu zaidi. Kwa mfano, mteja wa Bomba akilipia kifurushi
cha Family atazawadiwa kifurushi cha Compact. Mteja wa Family akilipia
Compact anapata kifurushi cha Compact+ na yule wa Compact akilipia
Compact+ anapewa kifurushi cha Premium”, alisema Shelukindo.
Aliongeza kuwa” Kampeni hii ya
“Step Up” itadumu kwa kipindi cha muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1
March 2019 hadi tarehe 30 Aprili 2019 na itawahusisha wateja wa Wateja
wote ambao akaunti zao hazijakatika vifurushi vya Bomba, Family pamoja
na kile cha Compact
No comments :
Post a Comment