
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani
msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa
marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wa pili kulia) wakimfariji mama Mzazi
wa marehemu Ruge Mutahaba, Christiana Mutahaba wakati walipokwenda
nyumbani kwao marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa
familia , Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba wakati alipokwanda
nyumbani kwao marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam kutoa pole kwa
familia, Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wakati alipokwenda
nyumbani kwao marehemu Ruge Mutahaba, Mikocheni jijini Dar es salaam
kutoa pole kwa familia , Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
………………..
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa
mbele kuwahamasisha
vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za
maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.
Ameyasema hayo leo (Jumatano,
Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi
na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya
Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu amesema vijana nchini
walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na
kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na
kiuchumi ili waweze kujitegemea.
Waziri Mkuu amesema msiba huo ni
wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali
kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia
kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa
Amesema marehemu Ruge katika
kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali,
kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha
vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.
Pia, Waziri Mkuu amesema historia
yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya
vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo
nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.
“Marehemu alikuwa akitoa hadi
fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao
hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli
mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”
Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa
wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla
waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha
kuondokewa na mpendwa wao.
No comments :
Post a Comment