Wednesday, February 27, 2019

7 WAFIKISHWA MAHAKAMANI NJOMBE KWA MAUAJI YA WATOTO


A
NJOMBE 
Jeshi la polisi mkoani Njombe limewafikisha mahakamani watu saba kwa tuhuma za kuhisishwa na mauaji ya watoto nane yaliyoanza kutekelezwa tangu desemba 2018 akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 15 anaefahamika kwa jina la DAVID KASILA anaedaiwa kuhusika na mauaji ya watoto watatu wa familia tofauti katika nyakati tofauti.
Watu wengine ambao uchunguzi wa awali  umebainisha kuhusika na kufikishwa mahakamani ni pamoja na Jeol Nziku ,Nasson Kaduma na Alphonce Edward ambao wametekeleza mauaji ya watoto watatu wa familia moja, huku wengine wakiwa ni Maliana Malekela ,Edwini Malekela na Karitus Malekela ambao wanadaiwa kuhusika na mauaji ya mtoto Rachel Malekela. 
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa mkoa wa Njombe Rennata Mzinga amesema jeshi liliwakamata na kuwahoji watu 49 kuhusiana na mauaji hayo na kudai kwamba katika idadi hiyo saba ndiyo waliobainika kuhusika na mauaji hayo kwa sababu mbalimbali ikiwemo visasi, ugomvi wa mashamba pamoja na ramri chonganishwi ambapo katika kudhibiti ukatili huo jeshi liliwakamata na kuwahoji baadhi ya waganga, wafanyabishara na baadhi ya wanafamilia walio uliwa wapendwa wao.
Mbali na kuwafikisha watu saba mahakamani ,jeshi limeendelea na mchakato wa kuwabaini wahusika wengine huku likitoa rai kwa wananchi kutuma jumbe za kweli kituo cha polisi kuhusu wanaohusika na matukio hayo kwa kuwa kumekuwa na baadhi ya wananchi wanatuma jumbe za uongo hatua ambayo inaleta athari kiuchunguzi.
Watoto 8 wameuwawa njombe tangu mauaji ya watoto yaanze kutekelezwa.

No comments :

Post a Comment