Thursday, January 31, 2019

TAASISI YA WAHASIBU WANAWAKE (TAWCA) YAMWAGA VITABU VYA HESABU SHULE YA SEKONDARI TURIANI WILAYA YA KINONDONI


1
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa Taasisi ya TAWCA  Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant  kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Triani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
2 3
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa Taasisi ya TAWCA  Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant  kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) wa pili kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi boksi la vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Triani wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam na mmoja wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo  ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
4
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa Taasisi ya TAWCA  Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant akikabidhi vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Turiani Wilayani Kinondoni  kushoto ni Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA)  na wanachama wenzao wakishuhudia tukio hilo.
5
Wanachama wa Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant (TAWCA)wakiwa katika picha na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu hivyo.
6
Wanachama wa Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant (TAWCA) wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo.
…………………………………………………………………………………………
TAASISI ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA)wametoa msaada wa vitabu mbalimbali vya hesabu na masomo ya biashara vyenye thamani ya Sh.milioni 8.5 kwa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam.
Uamuzi wa TWCA kutoa msaada huo kwenye shule hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi hasa
wa kike kupenda masomo ya hesabu nchini ili baadae waje kuongeza idadi ya watalaamu wahasibu nchini.
Akizungumza leo shuleni hapo wakati wa tukio la kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania Tumaini Lawrence amesema wanawake wahasibu nchini wameona haja ya kushiriki kwa vitendo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo yanayohosu hesabu na ndio maana wameamua kutoa msaada huo wenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu.
“Wanawake wahasibu nchini kwa umoja wetu tumeamua kuchangishana fedha ili kufanikisha msaada huu kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari ya Turiani.Tumekuja kuwahamasisha wasome kwa bidi masomo ya hesabu na biashara ili tuongeze idadi ya wahasibu na hawa wahasibu wa kike katika nchi yetu ambapo kwa sas idadi yao ni chini ya asilimia 25 ya wahasibu wote.
“Kuna dhana ambayo inajengeka kuwa masomo ya hesabu ni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume tu lakini sisi wahasibu wanawake ambao ndio mama zenu tunawaambia wanafunzi kuwa somo la hesabu ni la wote.Hivyo wanafunzi wa kike jitahidi kusoma hesabu na masomo ya biashara,”amesema Lawrence.
Kuhusu mikakati ya taasisi ya wahasibu nchini, Lawrence amesema ni kuendelea kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya hesabu na huku akitoa ushauari kwa wazazi na walezi kuwajengea uwezo wa kujiamini watoto hao.
“Naomba nisieleweke vibaya ila wahasibu wanawake wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi wanakuwa waaminifu sana.Kwa kutambua hilo ni jukumu letu kuwatia moyo wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu,” Lawrence.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Neema Msusa amesema ni faraja kwao kufika shuleni hapo kuzungumza na wanafunzi hao.
“Tumefika shuleni hapa kwa lengo la kumsha ari kwa wanafunzi wetu wa kike kusoma masomo ya biashara.Tunawaambia hesabu haikimbiliki, hivyo wasome kwa bidi kwani tunaona faida ya kusoma hesabu maana wanawake wahasibu kila mmoja yupo kwenye taasisi anafanya kazi yake vizuri,”amesema
Ameongeza wao kuwa wahasibu kumetokana na msingi mzuri ambao uliwekwa na walimu wao kuanzia ngazi ya chini , hivyo wanaamini wanafunzi wa kike watasoma kwa bidi masomo ya hesabu.
Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam Angalo Izungo amesema anashukuru kupata msaada huo na kwamba wahasibu hao wanawake wameonesha upendo wa dhati kwa shule yao.
Amefafanua changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni vitabu vya masomo ya hesabu na biashara pamoja a uhaba wa walimu , hivyo baada ya kupata vitabu ombi lao ni Serikali kuwapatia walimu kwani waliopo ni wawili tu na wanafunzi walionao ni 506.
“Tunao walimu wawili tu wa masomo ya hesabu hapa shuleni kwetu, hivyo tunashukuru kwa msaada huu.Tunaomba Serikali yetu ituongezee walimu wa masomo ya hesabu shuleni kwetu, wanafunzi wetu wanapenda hesabu sana,”amesema Izungo.

No comments :

Post a Comment