Thursday, January 31, 2019

TAASISI YA OCEAN ROAD YATOA MAFUNZO KWA MADAKTARI WA SARATANI KUTOKA NCHI ZA AFRIKA


k01
Mkurugenzi wa ORCI, Mkurugenzi wa Mipango hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Dk.Daudi Maneno akizungumza wakati akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu magonjwa ya saratani iliyofanyika leo hospitalini hapo jijini Dar es salaam  kushoto ni Dk. Maguha Stephano.
k1
Mkurugenzi wa Kinga na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani ORCI, Crispin Kahesa akitoa mada  katika semina hiyo iliyofanyika leo kwenye hospitali ya Ocean Road.
k2 k3
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Saratani Dk.  Sikudhani Muya akitoa mada kwa waandishi wa habari wakati wa semina hiyo.
……………………………………………………………………………….
Mkurugenzi wa Kinga na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani ORCI, Crispin Kahesa amesem taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi cha Muhimbili imefanikiwa  kutoa mafunzo kwa wanafunzi 38 wa Shahada ya Kwanza ya Tiba ya Mionzi (Bachelor of Science in Radiation Therapy Technology) huku ikitoa  mafunzo  wanafunzi 26 wa Shahada ya Uzamili ya Onkolojia (Masters of Medicine in Clinical Oncology).
Daktari Crispin Kahesa  ameyasema hayo leo Januari 31, wakati wa akiwasilisha mada kwenye semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani iliyofanyika hospitalini hapo.
Amesema mafunzo hayo yameongeza uwepo wa wataalamu wa huduma za Saratani katika taasisi  hapa nchini ambapo  kwa sasa Taasisi ina madaktari bingwa wa Onkolojia 25, ikilinganishwa na madaktari bingwa 5 waliokuwepo mwaka 2010.
“Kuanzishwa kwa programu ya Shahada ya Uzamili ya Onkolojia (Masters of Medicine in Clinical Oncology) nchini kumeongeza ushirikiano na nchi za nje ambazo zimekuwa zikileta  wanafunzi kwa ajili ya mafunzo mbalimbali hapa nchini” Ameongeza  .
Amesema hadi kufikia Desemba 2018 programu hiyo  ilikuwa imefundisha madaktari 17  ambapo kutoka  nchini  Kenya walikuwa  (8) kutoka  Rwanda walikuwa  (5), DRC alikuwa mmoja (1), Nigeria alikuwa mmoja (1), Ethiopia mmoja (1), na Comoro alikuwa mmoja (1) pia.
Taasisi ya Ocean Road pia imetumia wigo huo wa ushirikiano kutangaza huduma mbalimbali  zinazotolewa hapa nchini  hivyo kuvutia wagonjwa kutoka nchi hizo kuja nchini kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.
“Tunajukumu la kuhakikisha tunatoa huduma za kinga na tiba na kutoa elimu kwa umma ya kujikinga na magonjwa haya na kuendesha program za mafunzo kwa wataalamu na kufanya tafiti mbalimbali,” amesema.
Amesema eneo jingine ambalo serikali imewekeza ni upande wa tiba ambapo sasa wamepata mashine ya LINAC zinazotibu kisasa zaidi magonjwa hayo katika mfumo wa 3D.
“Matokeo ya tiba kwa mashine hizi ni bora zaidi kuliko mashine ambazo tulikuwa tunazitumia hapo awali, tumeweza kupunguza muda wa magonjwa kisubiri matibabu kutoka wiki sita hadi chini ya wiki nne,” amebainisha.
Ameongeza “Haya ni mafanikio makubwa kwetu, kuweza kuendelea kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma.
Daktari Crispin Kahesa ameongeza kuwa wanaishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali na kutoa fedha ili kuwezesha taasisi ya (Ocean Road Cancer Intitute) kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi jambo ambalo linawajenga kiutendaji na kuwapa hamasa ya kuchapa kazi.
Naye daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani ORCI, Maguha Stephano amesema maadhinisho ya Siku ya saratani hufanyika Februari 4, kila mwaka.
“Hupewa kauli mbiu kwa kipindi cha miaka mitatu mitatu, kwa mwaka 2019 hadi 2021 inasema ‘Mimi Ninaweza, Nitapiga Vita Saratani’, katika kuiadhimisha tunafanya uchunguzi wa awali bila malipo, tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuja kujua afya zao,” amesema.

No comments :

Post a Comment