Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiangalia tiles katika jengo la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akipita katika moja ya maeneo ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali
wa Mtumba mkoani Dodoma alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi
zinazosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Wanaomfuatia kwa
nyuma ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba Dkt Sophia Kongela na
Mkurugenzi Dkt Maulid Banyani.
Meneja
wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Serikali kutoka Shirika la Nyumba la
Taifa Haikameni Mlekio akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika
la Nyumba Dkt Sophia Kongela na Mkurugenzi wa NHC Dkt. Maulid Banyani
maendeleo ya ujenzi katika ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali Mtumba
mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiangalia shimo la choo katika wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa
ofisi za Serikali katika Mji wa Ser
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiingia katika jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara wakati akikagua
maendeleo ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani
Dodoma, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba Dkt Sophia
Kongela na kushoto ni Mkurugenzi Dkt Maulid Banyani.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiangalia moja ya vyumba katika ofisi zinazojengwa katika Mji wa
Serikali Mtumba mkoani Dodoma wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa
ofisi hizo.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiangalia madirisha ya nondo ambayo yako tayari kupachikwa wakati
akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za serikali katika eneo la Mtumba.
Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiingia katika eneo la jengo la Wizara ya Fedha na Mipango alipowasili
kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi zinazojengwa na Shirika la Nyumba
la Taifa katika Mji wa Serikali Mtumba, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya
NHC Dkt Sophia Kongela na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la
Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
…………………………………………………………………………………
Na Munir Shemweta, DODOMA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amechochea kasi ya ujenzi wa ofisi za serikali katika eneo la Mtumba
mkoani Dodoma unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Kasi
hiyo inatokana na ziara za mara kwa mara zinazofanywa na Naibu Waziri
huyo wa Ardhi katika eneo hilo kwa nia ya kuhakikisha ujenzi wake
unakamilika katika muda uliopangwa.
Akiambatana
na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa .Dkt Sophia Kongela
pamoja na Mkurugenzi wa Shirika Dkt Maulid Banyani jana, Naibu waziri
Mabula alijionea maendeleo makubwa ya ujenzi huo ambapo sasa umefikia
hatua ya kuezeka.
Mbali
na kufikia hatua hiyo, kazi nyingi katika ujenzi huo zinaenda kwa
pamoja kama vile kuweka njia za umeme, tiles, utengenezaji madirisha ya
nondo pamoja na mashimo ya choo jambo
linaloonesha Shirika limejipanga kukamilisha kazi mapema tofauti na
makampuni mengine ya ujenzi yanayofanya kazi kwenye eneo la Mtumba.
Kampuni
ya Ujenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa katika eneo hilo la Mtumba
inajenga majengo ya ofisi nne za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maenendeleo
ya Makazi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Nishati pamoja na
Wizara ya Fedha na Mipango.
Akizungumza baada
ya kukagua kwa mara ya pili ujenzi wa ofisi hizo, Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula alisema kasi inayooneshwa na
Shirika la NHC katika ujenzi huo ni ishara tosha kuwa shirika hilo
kupitia kampuni yake ya ujenzi lina uwezo mkubwa wa kujenga majengo kwa
haraka na yenye viwango.
Alisema,
hata kama ujenzi wa ofisi zinazosimamiwa na shirika hilo katika eneo la
Mtumba utachelewa kidogo lakini ucheleweshaji huo utatokana na MHC
kutaka kujenga majengo ya uhakika na yenye ubora unaotakiwa.
Dkt
Mabula ameendelea kutoa sifa kwa Ofisi ambazo majengo yake yanasimamiwa
na shirika la Myumba la Taifa kutokana na ukaribu inaouonesha katika
kipindi chote cha ujenzi kwa nia ya kuwa na majengo yanayokidhi mahitaji
ya Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) na ofisi husika kwa kuwa mawazo ya
pande zote yatakuwa yamejumuishwa katika kutekeleza ujenzi huo.
No comments :
Post a Comment