Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
OFISI ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) imebaini matumizi mabaya ya fedha za serikali Sh. bilioni 2.98 katika halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wakuu wa idara wote waliohusika wavuliwe nyadhifa zao huku watumishi wengine waondolewe majukumu ili vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria dhidi yao.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa
nchi ofisi ya Rais Twala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Selemani
Jafo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya
uchunguzi
maalum uliofanywa kwa halmashauri ya wilaya hiyo.
Jafo alisema kuwa Ofisi ya Rais
Tamisemi imefanya uchunguzi maalum katika halmashari 12 nchini ambazo ni
Ulanga, Same, Mbulu, Meru, Itigi, Misungwi, Nyang’hwale, Serengeti,
Bahi, mpwapwa, Morogoro Dc na Kibaha Tc ambapo katika halamasahuri ya
Ulanga uchuguzi ulianza Novemba 13 hadi 23 mwaka huu.
Alisema uchunguzi huo ulifanyika
kufuatia malalamiko ya wanachi mbalimbali pamoja na mbunge wa jimbo la
Ulanga Mhe. Goodluck Mlinga kutokana na ubadhirifu uliokuwepo.
Aidha alisema kiasi hicho
kimebainika kupotea kutokana na matumizi mabaya ya fedha za serikali
ambapo watumishi wasio waadilifu katika halmashauri hiyo walikiuka
taratibu na kufanya manunuzi hewa na kutumia vibaya fedha kinyume na
malengo yaliyopangwa.
“Halmashauri hii imekuwa ikifanya
udanganyifu katika taarifa za miradi ya maendeleo taarifa za mfuko wa
wanawake na vijana, kwa ujumla inausimamizi mbovu wa mapato na kuwa na
udhibiti hafifu wa makusanyo na matumizi ya fedha za Umma”alisema Jafo.
Jafo alisema kuwa mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Ulanga, Yusufu Daud Semguruka kwa nafasi yake
ya afisa masuhuli alishindwa kusiomamia sheria ya fedha za serikali za
mitaa katika kudhibiti na kuweka mifumo dhabiti ya kuhakikisha fedha
ziko salama kuanzia makusanyo hadi matumizi yake.
“Hii ni pamoja na kushindwa
kumsimamia mweka hazina wa halmashauri katika kutekeleza majukumu yake
na kwa kushindwa kutekeleza majuku hayo amesababisha hasara halmashauri
ya shilingi 2,980,172,763.60″alisema Jafo.
Alifafanua kuwa Rajabu
Siriwa,ambaye alikuwa ni mweka hazina wa halmasahuri hiyo alichangia
kuhujumu mapato ya serikali kwa kuweka utaratibu ambao umeisababishia
hasara serikali.
Alisema kuwa mweka hazina huyo
aliidhinisha malipo ya sh. 225,586,400 nje ya bajeti bila idhini ya
ofisi ya Rais Tamisemi ambapo malipo hayo yalihusisha posho ya safari ya
mkurugenzi mtendaji Sh. 192,000,000.
“Pia kukusanya mapato na
kutoyapeleka benki, katika mfumo wa LGRCIS umeonyesha halmashauri
ilikusanya fedha ambazo hazikupelekwa benki kabisa shilingi
760,686,732.43 fedha hizi hazijulikani matumizi yake halisi ni
nini”alihoji Jafo.
Aidha alisema kuwa mweka hazina
huyo aliandaa taarifa zenye udanganyifu kwa utekelezaji wa miradi ya
maendeleo inayotumia fedha za makusanyo ya ndani.
“Halmashauri imeripoti kupeleka
shilingi 301,442,686 uhalisia wamepeleka 113,406,106.34 na udanganyifu
katika mfuko wa vijana na akina mama halmashauri inaripoti kupeleka
shilingi 120,000,000 uhalisia wamepeleka sh. 31,500,000 kwa mwaka
2017/18 na 2018/19 hadi novemba 2018 wakati uchunguzi
unakamilika”alisema
Aidha Jafo alisema kuwa Mhandisi
David Kaijage akiwa anakaimu ofisi ya mkurugenzi februari mosi mwaka huu
hadi Februari nane alihusika kwenye kuihujumu halmashauri kwa mapato ya
Sh. 470,000,000 yaliyopolelewa kutoka kiwanda cha kilombero Valley Teak
Company kwa kuzirejesha kwa mlipaji siku hiyohiyo waliyopokea.
“Pia alisaini hati ya malipo kumlipa bahari Phamarcy kwa siku ambayo hakuwa kaimu mkurugenzi na mkurugenzi alikuwepo”alisema.
Wakati huo huo Bw. Stanley Godwil Nyange na Bw. Isaack Mwasankope Salumu ambao wote ni wahasibu wameihujumu Halmashauri kwa kutumia akaunti zao binafsi kupokea fedha za makusanyo ya Halmashauri kiasi cha sh 203.398,700 aliongeza.
Waziri Jafo pia alisema kuwa uchunguzi huo pia umebainisha kuwa Isaack Mwasankope, Salehe Mbogoso pamoja na Johson Mwanyombole ambao wote ni wahasibu wa halmashauri hiyo walihusika kuchukua fedha taslim za makusanyo katika kituo cha kivukoni na kisha kuzitumia bila kuzipeleka Benki sh 168,000,000.
Yassin Galahenga na Mohamed Majaliwa Saidi wataalam wa mifumo (TEHAMA) walishirikiana na wahasibu kurekebisha Ankara na kufuta madeni bila idhini ya Mkurugenzi alibainisha Waziri Jafo.
Waziri Jafo aliongeza kuwa Bw. Willy Ndabila ambaye alikua afisa manunuzi alihusika na manunuzi hewa ya madawa yenye thamani y ash. 73,212,909.40 pamoja na kulipa fedha zaidi yaani sh 146,425,818 huku Goodluck Mbata ambaye ni muhasibu wa hospital aliandaa malipo na kusainisha mara mbili kwa watu tofauti huku akijua kufanya hivyo ni kuandaa malipo mara mbili kwa hitaji moja (double paymet).

Waziri Jafo aliagiza ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhakikisha kuwa wakuu wa idara na vitengo
waliohusika akiwemo Willy Ndabila ambaye amehamishiwa itilima,na Rajabu
Siriwa ambaye amehamishiwa Gairo wavuliwe nyadhifa zao na mamlaka za
nidhamu na vyombo vya dola viendelee na hatua kwa mujibu wa sheria.
Aliongeza kuwa watumishi wote
waliohamishiwa Halmashauri ya ulanga wakiwa na makosa yaani DPMU Willy
Ndabila na DT Rajabu Siriwa warejee halamashauri ya Ulanga ili
kuiwezesha halmashauri na vyombo vya Dola kufanya kazi yake.
“Maelezo juu ya mkurugenzi huyu wa Ulanga yenyewe yatatolewa baadaye na serikali”alifafanua Jafo.

Hatahivyo Jafo alisema kuwa mkuu
wa mkoa wa Morogoro ahakikishe kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imepata
maelezo kwanini wataalamu hao hawakuchukuliwa hatua stahiki zenye tija
dhidi ya taarifa za mkaguzi wa ndani ya robo ya tatu ya mwaka wa
fedha2017/18 kabla ya januari 15 mwakani.

uchunguzi maalum uliofanywa kwa halmashauri ya wilaya hiyo.

No comments :
Post a Comment