Na MWANDISHI WETU -ZANZIBAR
MTOTO Manahil Mundhir Rashid
mwenye umri wa miaka mitano (pichani), amepotea kwenye mazingira ya
kutatanisha eneo la Mkunazini mjini Unguja Visiwani Zanzibar.
Baba wa mtoto Mundhir Rashid,
amesema kuwa mtoto wake alipotea Oktoba 14, mwaka huu baada ya kushuka
kwenye basi wakati akitoka shule.
“Nipo kwenye mashaka ni zaidi ya miezi miwili sasa sijamuona mtoto wangu
sijui yuko wapi na kwenye mazingira gani Mungu wangu.
“Binafsi nina mashaka makubwa na
usalama wa mtoto wangu na hata mimi na mke wangu. Tumejawa na hofu ni
wapi alipo mtoto wetu,” amesema Rashid
Kutokana na hali hiyo amesema
walitoa taarifa Kituo cha Polisi Madema mjini Unguja ambapo
lilifunguliwa jalada ya uchunguzi namba MAD/R.B 8011/18.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa
ya polisi ilieleza kuwa tayari mtu mmoja ameshakamatwa Oktoba 17, mwaka
huu katika Bandari ya Malindi, Zanzibar kwa kosa hilo la kudaiwa
kutorosha mtoto.
Baba huyo wa mtoto huyo aliwaomba
wananchi kwa yeyote atakayemuona atoe kituo kituo chochote cha polisi
kilicho karibu yake au awasiliane na baba mzazi wa mtoto huyo kwa namba
ya simu 0773044899
No comments :
Post a Comment