Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Stella Ikupa
Alex (kushoto) akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania
(TFB) Bi. Joyce Fissoo Cheti cha Kutambua mchango wa Bodi hiyo katika
kufanikisha Tamasha la KATAA MIHADARATI lililofanyika leo Tarehe
28.12.2018 katika viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es Salaam.
Tamasha hili limeratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Taasisi ya
Binti Filamu, pamoja na Tume yakudhibiti na kupambana na dawa za
kulevya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Stella Ikupa
Alex (wa tatu kushoto, walio kaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo
(anaefuata,kulia) Kamishna wa Kinga na Tiba Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya Dkt. Peter Patrick Mfisi na Mwenyekiti wa
Asasi ya Binti Filamu Bi. Ndumbagwe Misayo(Thea). Kushoto ni
Muwakilishi
wa Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Mburahati katika Tamasha la KATAA
MIHADARATI lililofanyika kwenye viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar
es Salaam. Tamasha hili lina lengo la kutoa Elimu kuhusu madhara ya Dawa
za Kulevya na limeratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Asasi ya
Binti Filamu, pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya.
…………………………
Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Bunge, Sera, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa Alex
ameitaka jamii kushiriki kwa pamoja katika mapambano na udhibiti wa Dawa
za kulevya kwa kuhakikisha kila raia mwema kwa nafasi yake anashiriki
katika kutokomeza uingiaji, usambazaji na matumizi ya dawa hizo
zinazoathiri nguvu kazi na kupelekea mzigo kwa Familia, Jamii na
Serikali.
Rai hiyo imetolewa leo katika
Tamasha la Kataa Mihadarati lililo ratibiwa na Asasi isiyo ya kiserikali
iitwayo Binti Filamu, Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Mamlaka ya
Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya na Shirika la Bima la Taifa (NIC)
lenye kauli mbiu isemayo “Nguvu yako, Afya yako, Jiokoe Uokoe Tanzania” lililofanyika katika viwanja vya Mburahati Barafu Jijini Dar es Salaam.
“Si Serikali pekee yenye dhamana
ya kupambana na Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini, bali ni jukumu la
kila raia mwema wa Tanzania kuhakikisha anatumia nafasi yake kwa kutoa
taarifa kwenye Mamlaka husika ili kuweza kudhibiti Uingia, Usambazaji na
Matumizi ya Dawa haramu za Kulevya” Alisema Mhe. Stella.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo alisema Sekta ya Filamu
na Michezo ya Kuigiza ni moja ya Sekta kubwa zinazopunguza tatizo la
ajira nchini ikiwa itatumiwa ipasavyo, hivyo Wadau wake wanatakiwa
kutojihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya kwani kufanya hivyo
kutawapotezea heshima katika jamii na kupelekea kujirudisha nyuma
kimaendeleo.
“Sekta ya Filamu ni Sekta Tajiri
sana na inahitaji Wadau wasio jihusisha na Dawa za kulevya kwakuwa
utumiaji wa Dawa hizo unarudisha nyuma utendaji kazi wao na kushindwa
kujikwamua kiuchumi”Alisema Fissoo.
Tumekubali kushirikiana na Binti
Filamu ambao ni Wadau wa Bodi kwa kuwa tunaona madhara ambayo yamegusa
Sekta ya Ubunifu Filamu ikiwemo. Tutaendelea kushirikiana nao ili kwa
pamoja tuokoe kizazi cha sasa na baadae. Ni wajibu wetu kumsaidia Mhe.
Rais na ameonesha dhamira ya dhati kuhakikisha Tanzania inaishi bila
Dawa za kulevya. Aliendelea Bi. Fissoo
Matumizi ya Dawa za Kulevya
yanapoteza ndoto za Vijana wengie hapa nchini wakiwemo Wadau wa Sekta ya
Filamu na Michezo ya Kuigiza ambapo wengi wao hujiingiza katika
matumizi ya Dawa hizo bila kujua madhara yake na baadae wanapata madhara
makubwa yakiwemo maambukizi ya magonjwa, kupoteza heshima na hata
kupoteza maisha.
No comments :
Post a Comment