Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi pamoja
na wafanyakazi wa machinjio ya Vingunguti wakati akitoa zawadi ya mwaka
mpya ya ng’ombe 20 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Hospitali ya Ocean Road, na hospitali za rufaa za Mkoa
wa Dar es Salaam ikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana na Mwananyamala.
Baadhi ya wananchi na maofisa wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakimsikiliza mkuu wa
mkoa kabla ya kutoa zawadi ya mwaka mpya.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali
Yacoub Hassan Mohamed akimshukuru Mh. Makonda kwa kulipatia jeshi hilo
zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Mhe. Makonda na Mkurugenzi wa
Rasilimaliwatu na Utawala wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bwana
Makwaia Makani
Mhe.
Makonda akikagua ng’ombe ambao ametoa zawadi ya mwaka mpya kwa
hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la polisi na Jeshi la Ulinzi
la Wananchi la Tanzania (JWTZ).
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza
katika mkutano huo baada ya kukabidhiwa zawadi ya ng’ombe 20 kwa ajili
ya mwaka mpya 2019. Katikati ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed na
Mhe. Makonda.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makonda kabla ya kutoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali hizo, JWTZ na jeshi la polisi.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe akimshukuru
Makonda kwa kutoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali za mkoa huo.
Baadhi ya ng’ombe wakiwa katika machinjio ya Vingunguti leo baada ya
Mhe. Makonda kukabidhi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt.
Grace Maghembe.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
………………………
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa zawadi ya ng’ombe
20 kwa ajili ya mwaka mpya 2019 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na hospitali za rufaa za
Temeke, Ilala na Kinondoni ikiwamo Taasisi ya Saratani Ocean Road
(ORCI).
Zawadi
hiyo imetolewa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo pamoja na
wafanyakazi ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza kutokana na huduma bora
ambazo wanazozitoa na hivyo kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Akizungumza
katika machinjio ya Vingunguti, Mkuu wa Mkoa Makonda
amewataka watumishi wa hospitali hizo kuongeza juhudi katika sehemu zao
za kazi ili Mkoa wa Dar es Salaam uwe namba moja katika kutoa huduma
mbalimbali za afya.
“Idadi ya malalamiko imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma za matibabu kuimarika,” amesema Makonda.
Pia,
mkuu huyo wa mkoa ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa Jeshi la Polisi na
ng’ombe 20 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili
ya sikukuu ya mwaka mpya 2019.
Katika
hatua nyingine, Makonda amesema kwamba Serikali itajenga machinjio ya
kisasa na kwamba ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 8.5.
Amesema
lengo la kujengwa kwa machinjio ya kisasa ni kupanua soko la nyama na
kwamba jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi huo litawekwa Januari mwakani.
Naye
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe amemshukuru
mkuu wa mkoa kwa kutoa zawadi ya mwaka mpya 2019 kwa kuwa itaongeza
uwajibikaji katika hospitali hizo.
Dkt.
Maghembe amesema katika juhudi za kuboresha huduma za afya kwa
wananchi, mkoa huo kwa kushirikiana na wataalam wa Muhimbili, Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na hospitali za wilaya wamefanikiwa
kupima afya zaidi ya wananchi 100,000 mkoani Dar es Salaam.
Pia, amemshukuru kiongozi huyo kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujifungua kwa kinamama wajawazito.
No comments :
Post a Comment