Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake
Vuga, Mjini Zanzibar, kuhusu kutunza amani wakati wa kuukaribisha mwaka
mpya 2019.
Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud
akizungumza kuhusu kutunza amani wakati wa kuukaribisha mwaka mpya
2019 huko Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar.
…………………………………………………………………..
Na Mwashungi Tahir
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wananchi wa Mkoa wa Mjini kujitokeza kwa
wingi katika ufunguzi wa kiwanja cha Mao Tse Tung likiwa ni
tukio la
Historia kwa hapa Zanzibar na linatarajiwa kufanyika tarehe 3/1/2019.
Akizungumza na waandishi wa
habari huko Ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumzia mafanikio
yaliyopatikanwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi kwa Mwaka 2018 na
kuukaribisha mwaka 2019 ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka
55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ikiwa ni muendelezo kila ifikapo
mwisho wa mwaka.
Alisema uzinduzi wa Mao Tse Tung
ni tukio la pili la Historia kwa Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo tukio
la mwanzo la historia ni Ufunguzi wa Uwanja wa Michezo Amani, na
kufunguliwa na Marehemu Mzee Amani Karume katika Mkoa huo.
Hivyo alisema miradi mengine 13
ni pamoja na ufunguzi wa Skuli ya Bwefum, uzinduzi wa bara bara kutoka
Fuoni mambo sasa na kwa mabata hadi kinuni , kituo maalum cha DNA ni
mashine ya kupimia minasaba kwa Mkemia Mkuu na kuweka jiwe la msingi
ZBS pia kutakuwa na makongamano .
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mambo mengi ya maendeleo
nchini kwa lengo la kuwataka wananchi wake waishi kwa amani na utulivu.
Pia amewaomba wananchi
washerehekee mwaka mpya kwa taratibu za jeshi la ulinzi na usalama
kwa amani bila ya uharibifu wa barabara, waepuke kuendesha vyombo kwa
mwendo wa kasi wakiwa wamelewa kwani kufanya hivyo kutaweza
kuwasababishia ajali na kuweza kupata ulemavu au kupoteza maisha .
“Nawaomba wale wenye kawaida ya
kuzunguka katika round about kwa fujo waache mara moja washerehekee
mwaka mpya kwa amani na utulivu kwani sehemu zote za Mkoa huu tumeweka
jeshi la ulinzi na usalama kwa lengo la kutaka wazanzibariA wote wawe
katika hali ya amani”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha akizungumzia mikakati ya
mwaka 2019 kuondoa kero kwa wananchi , shughuli za maendeleo za Serikali
na pia kutatua changamoto kwa wananchi wake ikiwemo madada poa kaka
poa na omba omba kuhakikisha wanaondoka kabisa .
No comments :
Post a Comment