Friday, December 28, 2018

NAIBU WAZIRI IKUPA AWAOMBA WADAU KUJITOKEZA MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA, AWAPONGEZA (NIC)


1
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC)  kutokana na mchango wa shirika hilo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival)  lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu inayoundwa  na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati Foundation  jijini Dar es salaam.
02
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti  Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi kutokana na mchango Mamlaka hiyo  katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival)  lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu Foundation inayoundwa  na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es salaam.
2
Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC)  akizungumza katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es salaam.
3
Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
4
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisoo akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
5
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akihutubia wananchi waliofika katika tamasha hilo kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.
6
Baadhi ya wasanii wa filamu wakifurahia baadhi ya burudani zilizokuwa zikitolewa katika tamasha hilo.
7
Baadhi ya waalikwa wakiwa katika tamasha hilo.
8
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikup kushoto, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo na Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi   wakipunga mikono yao juu wakati msanii Inspector Haroun hayupo pichani alipokuwa akitumbuiza katika tamasha hilo.
9
Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa katika tamasha hilo.
……………………………………………………………………………………………….
 Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana,Ajira na  Wenyeulemavu Stella Ikupa ameelezea jitihada zinazofanywa na  Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika kupambana na dawa za kulevya nchini na kwamba tatizo la dawa za  kulevya,kupongeza jitihada za wadau katika vita hiyo
liliwemo Shirika la Bima la Taifa (NIC) kutokana na udhamini wao katika tamasha hilo ambalo limelenga katika mapambano ya madawa ya kulevya.
“Tunawapongeza Binti Filamu kwa kuandaa tamasha hilo linalofahamika kwa jina la  Kataa mihadarati.Athari za dawa za kulevya kwa namna moja au nyingine  zinamgusa kila mtu kwenye jamii yetu.Serikali katika kuhakikisha inakomesha dawa  za kulevya iliamua kuunda mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za  Kulevya ambayo hakika imefanya kazi kubwa,”amefafanua Ikupa.
Ametoa ushauri kwa Binti Filamu kuhakikisha katika matamasha yanayokuja  waende kwenye mikoa ambayo athari za matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa na  kwa kufanya hivyo watasaidia kuikoa jamii kupitia elimu ambayo wanaitoa kuhusu
madhara yatokanayo na utumiaji wa dawa hizo. Kuhusu mapendekezo ambayo yametolewa na wadau mbalimbali kwenye tamasha  hilo yakiwemo ya Serikali kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu dawa za kulevya  amesema ameyachukua na watayafanyia kazi kwani ni mambo yanayowezekana.
Kwa upande wa Shirika  la Bima la Taifa Tanzania(NIC) limeshauri kwamba ufike wakati sasa  kuwepo na sera ambayo itahimiza mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kushiriki  kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vita ya dawa za kulevya nchini. Ushauri huo umetolewa leo Desemba 28,2018 na Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la  Taifa Tanzania(NIC) Israel Severe wakati wa tamasha la Kataa Mihadarati
liloandaliwa na Taasisi ya Binti Filamu chini ya Mwenyekiti wake muigzaji maarufu  wa filamu Ndumbagwe Misayo a.k.a Thea .Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo  alikuwa Naibu Waziri Stella Ikupa.
“Shirika la Bima la Taifa Tanzania tumeamua kushiriki kwenye tamasha hilo  kutokana na kutambua umuhimu wake kwa jamii.Tunajua moja ya jukumu letu ni  kushughulika na mambo ya bima lakini kwetu ni muhimu zaidi kuona jamii  tunayoihudumia inakuwa salama kiafya.Sote tunatambua athari za matumizi ya  dawa za kulevya, hivyo tumeamua kushiriki kikamilifu kwenye vita hii ili kukomesha  dawa hizo nchini.
“Tunashauri ifike wakati kuwe na sera ambayo itazungumzia umuhimu wa  mashirika na taasisi mbalimbali nazo kushiriki kwenye vita hii ya dawa za  kulevya.Hivyo ni wakati muafaka kwa Serikali kuweka sera itakayokwa chachu kwa  mashirika na taasisi zote kushiriki kwa vitendo na iwe ni wajibu wetu,”amesema  Severe.
Kuhusu tamasha hilo , Severe amesema anaupongeza uongozi wa Binti Filamu kwa  uamuzi wake wa kuandaa tamasha hilo lenye lengo la kutoa elimu kuhusu madhara  ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwamo  wao ambao wamedhamiria kwa dhati kukomesha dawa hizo nchini kwetu.
“Tunawapongeza Binti Filamu kwa kuandaa tamasha hilo ambalo kwetu sisi tunaona  ni mwanzo mpya kwa wasanii kuamua kushirikiana na wadau wengine kukomesha  dawa za kulevya.Wanastahili kuendelea kuungwa mkono na sisi NIC tutaendelea  kuwaunga mkono kadri watakavyokuwa wanaandaa matamasha haya ya kukataa  mihadarati,”amesema Severe.
Wakati huo huo Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba ambaye  pia ni Katibu wa Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam amesema umefika wakati  wa kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli katika mapambano dhidi ya  dawa za kulevya.
Amesema kuna wasanii wengi wamekuwa wakijihusisha aidha kutumia dawa za  kulevya au kugeuzwa makontena wa kubeba dawa hizo kwa maslahi ya  wafanyabiashara lakini madhara yake ni makubwa, hivyo umefika wakati wa  kukataa kuwa sehemu ya makontena na watumiaji wa dawa hizo.
Akizungumzia tamasha hilo msanii wa muziki wa Bongo Fleva Haruna Kahena  Inspekta Haroun amesema kitendo cha Binti Filamu kuandaa tamasha hilo ni wazi  wameonesha dhamira njema ya kupambana na dawa za kulevya ambapo kwa  sehemu kubwa wapo baadhi ya wasanii wamekuwa wakiyatumia.

No comments :

Post a Comment