Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua uboreshaji wa Mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangali
jijini Dodoma, wakati alipokagua Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya
Kimkakati katika Jiji hilo, Desemba 29, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la
Dodoma, Gowin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala
jijini Dodoma, wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya
Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Watatu kushoto ni
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony
Mavunde na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin
Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala
jijini Dodoma wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya
Kimkakati katika jiji hilo, Desemba 29, 2018. Watatu kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la
Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa
jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi
lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa
katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Mheshimiwa
Majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua Mradi wa Uendelezaji Miji ya
Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Wengine pichani
kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa ametembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika
jiji la Dodoma na kukagua ujenzi wa maegesho ya malori makubwa katika
eneo la Nala
na uboreshwaji wa mandhari ya eneo la kupumzikia la
Chinangalijijini Dodoma.
Pia amemuagiza Mkurugenzi wa jiji
la Dodoma, Godwin Kunambi andelee kutenga maeneo ya mapumziko ili
wananchi wapate sehemu za kukutana na kubadilishana mawazo baada ya
kumaliza kufanya kazi.
Waziri Mkuu amekagua maeneo hayo
leo (Jumamosi, Desemba 29, 2018) ambapo ameupongeza uongozi wa jiji la
Dodoma kwa kubuni wazo hilo na kusema kwamba ni muhimu kwa miji mikubwa
kutenga maeneo ya kwa ajili ya mapumziko.
Amesema lazima jiji la Dodoma
lipangwe kisasa na amewataka wahandisi wahakikishe maeneo ya mapumziko
yatengwa na yanatumika kama ilivyokusudiwa. Pia amemtaka Mkurugenzi wa
Jiji, Kunambi aendelee kusimamia ujenzi wa kimkakati ndani ya jiji hilo.
”Hatuwezi kuwa tumejaza nyumba
kila eneo, watu hawana mahali pa kupumzika na kukutana na marafiki zao
plan ya Chinangali Park ni nzuri, Jiji la Dar es Salaam plan ya awali
kulikuwa na maeneo ya mapumziko lakini watu wa Idara ya Ardhi
waliyauza.”
Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu
amekagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi
wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la
wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya
tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema ameridhishwa
na utekelezwaji wa agizo lake baada ya kutembelea eneo hilo na kukuta
uzio umebomolewa na sasa kuna bustani iliyojengwa kwa ajili ya mapumziko
na pia barabara imefunguliwa na wananchi wanaendelea kuitumia kama
ilivyokuwa awali.
Uzio huo ambao mbali na kujengwa
katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto kwenye
mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia uliziba barabara ya tisa, hivyo
kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Waziri Mkuu ameendelea
kusisistiza uongozi wa jiji kutenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya
matumizi mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za
jamii, viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Jiji la Dodoma amesema jiji la Dodoma ni miongoni mwa majiji manane
nchini yanayotekeleza mradi wa uboreshaji wa miji ya kimkakati
unaofadhiliwa na Serikali kupitia mkopo wa Benki ya Dunia.
Amesema katika jiji la Dodoma
mradi huo unahusisha ujenzi wa miundombinu ya barabara katika maeneo ya
Kikuyu, Chidachi, Kinyambwa, Itega, Njedengwa, Mapinduzi, Ilazo,
Ipagala, Chamwino, Kilimani, Majengo, Mlezi pamoja na maingilio na
stendi kuu ya mabasi na soko kuu zenye jumla ya urefu wa kilomita 26.6.
Mkurugenzi huyo amesema barabara
hizo zinajengwa kwa kiwango cha lami, pia zitawekwa taa za barabarani
takriban 925 zinazotumia mfumo wa umeme wa jua. Hata hivyo mradi huo
utahusisha ujenzi wa kituo cha maegezo ya malori makubwa takribani 300
katika eneo la Nala.
Ameongeza kuwa mradi huo
unahusisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi na soko kuu katika eneo la
Nzuguni, ujenzi wa vituo sita vya watembea kwa miguu, ujenzi wa vizimba
saba vya kukusanyia taka ngumu, uboreshaji wa mandhali ya eneo la
kupumzikia katika eneo la Chinangali na ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua
wenye urefu wakilomita 6.5 katika eneo la Ipagala.
No comments :
Post a Comment