Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB
Bw. Abdulmajid Nsekela akijaza fomu ili kuweka fedha kwenye akaunti ya
Junior Jumbo kayika gari maalum la Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya Twende 9nteen JJ aliyoizindua leo katika viwanja vya Mlimani
City jijini Dar es salaam ili kuwahamasisha wazazi kuwafungulia akaunti
hiyo watoto na kuwawekea akiba kwa ajili ya elimu katika siku za usoni
waliosimama nyuma yake kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na
Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB Bi. Tully Esther Mwambapa, Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji na Huduma kwa wateja Dkt. Joseph Witts
na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka wakishuhudia tukio hilo.
Bw. Abdulmajid Nsekela
amewahimiza wazazi na walezi wa watoto kuwafungulia watoto akaunti ya
Jumbo Junior na kuwawekea akiba kwa ajili ya maisha ya baadaye likiwemo
suala zima la elimu.
Mkurugenzi huyo wa Benki ya CRDB
amezungumza hayo wakati akizindua kampeni ya Twende9nteen JJ yenye lengo
la kuwahamasisha wazazi kuwawekea watoto wao akiba kidogokidogo kwa
ajili ya kuwasiadia katika elimu na mambo mbalimbali katika siku za
usoni.
Ameongeza kuwa mzazi unaweza
kuamua kumuwekea mtoto hata shilingi 5000 kwa siku ambapo kwa mwezi
atakuwa umemuwekea kwenye akautni kiasi cha shilingi 150.000 na hiki
nikiwango kikubwa siyo sawa na kutomuwekea mtoto akiba yoyote.
“Nawaasa wazazi tujenge tabia ya
kuwafundisha watoto wetu kuweka akiba kwa kuwawekea akiba kidogokidogo
jambo ambalo litawafanya kujifunza pia kuwa na tabia ya utunzaji mzuri
wa fedha zao mara watakapokuwa watu wazima.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB
Bw. Abdulmajid Nsekela akikabidhiwa risiti yake mara baada ya kuweka
fedha kwenye akaunti ya Junior Jumbo katika gari maalum la Benki ya
CRDB wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Twende 9nteen JJ aliyoizindua leo
katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam ili kuwahamasisha
wazazi kuwafungulia akaunti hiyo watoto na kuwawekea akiba kwa ajili ya
elimu katika siku za usoni waliosimama nyuma yake kutoka kushoto ni
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji na Huduma kwa wateja Dkt. Joseph
Witts na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka wakishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB
Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza na watoto waliofunguliwa akaunti za
Junior Jumbo na wanaotarajiwa kufunguliwa akaunti hiyo wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya Twende 9nteen JJ aliyoizindua leo katika viwanja
vya Mlimani City jijini Dar es salaam ili kuwahamasisha wazazi
kuwafungulia akaunti hiyo watoto na kuwawekea akiba kwa ajili ya elimu
katika siku za usoni
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na
Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Bi. Tully Esther Mwambapa akiwa pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
Twende 9nteen JJmlimani City jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya watoto wenye akaunti za
Junior Jumbo wakifurahia jambo huku wakipunga juu mikono yao wakati wa
uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akicheza muziki na watoto katika uzinduzi huo.
Watoto wakicheza muziki.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji na Huduma kwa wateja Dkt. Joseph Witts kulia na Naibu
Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka
wakishuhudia tukio hilo wakicheza na watoto katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kampeni hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na
Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Bi. Tully Esther Mwambapa akishiriki
kucheza na watoto walioletwa na wazazi wao katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akiwa katika picha ya pamoja na watoto.
No comments :
Post a Comment