Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama mnavyofahamu linashiriki Ulinzi wa Amani ndani na nje
ya Bara la Afrika.JWTZ linasikitika kuwataarifu kwamba limewapoteza
wapiganaji wake watatu (3) waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa
Amani baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.
Mashujaa wetu waliouwawa ni Koplo
Mohamed Mussa, Koplo Erick Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya. Miili ya marehemu hao tayari imepokelewa
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuhifadhiwa katika
Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa mashujaa wetu hao zitatolewa katika sehemu
ya kuagia Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kesho tarehe 23 Novemba 2018 kuanzia saa 2.30
asubuhi. Vyombo vya Habari na Wananchi
wanakaribishwa tuungane katika kuaga mashujaa wetu.
Mungu azilaze Roho za
Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina.
No comments :
Post a Comment