Naibu Katibu Mkuu Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili na Utalii, Uvuvi na Mifugo kutoka
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Islam Seif Salum akifungua
mkutano wa wadau uliojadili masuala ya uchumi endelevu wa Bahari
‘Sustainable Blue Economy’ unaotarajiwa kufanyika Nchini Kenya. Kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said.
Mmoja wa washiriki wa Kikao hicho
Balozi Celestine Mushi kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara akichangia
jambo katika mkutano wa wadau uliojadili masuala ya uchumi endelevu wa
Bahari ‘Sustainable Blue Economy’
Prof. Kassim Kulindwa kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam akitoa majumuisho ya mkutano huo ulifanyika
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………
Katika jitihada za kujenga uelewa
juu ya dhana nzima ya uchumi endelevu utokanao na rasilimali za
bahari, mabwawa na mito Ofisi ya Makamu wa Rais imeendesha kikao cha
wadau kutoka taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na sekta ya uvuvi na
mazingira kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar ili kwa pamoja kuandaa
msimamo wa Nchi katika Mkutano unaotarajiwa kufanyika Nchini Kenya hivi
karibuni.
Akifungua kikao hicho Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili na Utalii, Uvuvi na Mifugo
kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Islam Seif Salum amesema
kuwa ni muhimu kwa Tanzania kama nchi kunufaika ipasavyo na fursa za
uchumi endelevu wa bahari katika nyanja za uvuvi, utafiti na uchimbaji
wa mafuta na gesi na katika sekta ya utalii.
“Tuko hapa kujadiliana na kuweka
mikakati ya pamoja kama nchi katika kuelekea Mkutano mkubwa wa masuala
ya kunufaika na rasilimali za uvivu katika bahari, mito, maziwa na
mabwawa, dhana hii ni mpya hapa nchini kwetu ingawa tunatekeleza kwa
kiwango kidogo.” Alisisitiza Dkt. Salum.
Dkt. Salum amesema kuwa mkutano
huo utajenga fursa zaidi za kuwekeza katika rasilimali za baharini ili
kutimiza lengo la kukuza uchumi na kuendeleza Tanzania ya Viwanda.
Kwa upande mwingine Afisa Uvuvi
Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Emelda Teikwa amesema kuwa dhana
ya ‘Blue Economy’ ni ngeni hapa nchini ila ni muhimu sana katika
uchumi. “Tunaangalia namna ambavyo Uchumi wa bahari unaweza kuchangia
katika kukuza pato la Taifa, kwa kuwa na uvuvi endelevu na kukuza sekta
ya utalii”. Alisisitiza Bi. Teikwa.
Tanzania ni miongoni mwa nchi
zitakazoshiriki katika Mkutano Mkubwa wa uchumi endelevu wa Bahari
‘Sustainable Blue Economy’ unaotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwishoni
mwa mwezi huu.
No comments :
Post a Comment