Na Shamimu Nyaki
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza
kuwa sekta ya filamu ni kiwanda mtambuka hasa katika uandaaji,
urushwaji, uuzaji na usambazaji wa maudhui .
Hayo
ameyasema leo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu uzinduzi wa jukwaa la maudhui linalotarajiwa kufanyika
Novemba 28 hadi 30 ,2018 Jijini Dar es Salaam.
“
Jukwaa hili lina umuhimu kwa kuimarisha maudhui na usambazaji
uliobora kwa kiasi kikubwa katika kupata taarifa muhimu ikiwemo
upatikanaji wa vifaa bora ili kuandaa kukidhi viwango vya kimataifa”
amesema Dkt. Mwakyembe.
Amezidi
kueleza kuwa kupitia jukwaa hilo litatoa fursa nzuri ikiwemo mijadala
mbalimbali ya namna ya kutatua changamoto zinazowakabili waandaji wa
maudhui wakiemo wa televisheni, redio pamoja na tasnia ya filamu .
Aidha
Dkt. Mwakyembe ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa filamu nchini
kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika jukwaa hilo ili kutoa maoni
yao kwa ajili ya kuboresha maudhui.
Naye
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe
amesema kuwa maudhui bora yanasaidia katika kukuza lugha ya Kiswahili
na kuongeza idadi ya vyombo vya habari vya mtandao vinavyosaidia
katika kurusha matangazo hayo ndani na nje ya nchi.
Kwa
Upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Juliana Shonza ameeleza kuwa Serikali iko tayari kuhakikisha
inashirikiana na jukwaa la maudhui pamoja na wadau wote wa tasnia ya
filamu ili kupata soko bora nje ya nchi.
Vilevile
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya Clouds Plus Production Bw.
Ramadhani Bukini anafafanua kuwa uanzishwaji wa Jukwaa la Maudhui ni
mpango wa kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa maudhui bora, kwa kutoa
elimu kwa waandaaji na wasambazaji wa maudhui nchini.
Jukwaa
la Maudhui linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 28 hadi
30 , 2018 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo litahusisha
midahalo na utoaji wa mada mbalimbali kutoka kwa wataalam waliobobea.
No comments :
Post a Comment