Naibu Waziri wa Madini Doto
Biteko, akionesha taarifa ya utafiti wa jiokemia uliofanywa nchi mzima
na Taasisi ya Jiolojia ya Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na
Taasisi ya Jiolojia ya China. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Jiolojia ya China Profesa Sun Xiaoming na Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Madini, Mathias Absai.
Naibu Waziri wa Madini Doto
Biteko katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya Jilojia ya
China, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), na
Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.
Naibu Waziri Doto Biteko
akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun
Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na kukamilika kwa utafiti wa
Jiokemia uliofanywa nchini.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming (kulia) akitoa taarifa ya
utafiti huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na kushoto
ni Kaimu Katibu Mkuu, Mathias Abisai.
Sehemu ya Wataalam kutoka
Taasisi ya Jiolojia ya China, Wizara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa
Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini wakifuatilia kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa GST, Yokobeth Myumbilwa akizungumza jambo katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Madini Doto
Biteko akizungumza jambo (katikati). Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi
ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming na kushoto ni Kaimu Katibu
Mkuu Mathias Abisai.
Naibu Waziri wa Madini Doto
Biteko akionesha Taarifa ya Utafiti wa Jiokemia iliyofanywa katika Mkoa
wa Mbeya. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China,
Profesa Sun Xiaoming na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Mathias Abisai.
…………………..
GST YAAGIZWA KUANDAA RAMANI ZA MADINI NGAZI ZA MIKOA, WILAYA
*Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika
Na Asteria Muhozya, Dodoma
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti
wa Madini Tanzania (GST) imetakiwa kuandaa ramani zinazoonyesha madini
mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ili kuwapa nafuu watanzania
wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kupokea taarifa ya Utafiti wa
Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo (Geochemical Mapping for High
and Low Density) uliofanyika nchi nzima kwa ushirikiano kati ya GST na
Taasisi ya Jiolojia ya China.
Naibu Waziri Doto pia, ameitaka
taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia serikali katika kupata
matokeo chanya katika shughuli za madini huku ikiongeza thamani ya kazi
kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST inaweza kutumia utafiti
huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi za Mikoa na Wilaya.
Akizungumzia manufaa ya tafiti
huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu watanzania wanaofanya
shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji wa uhakika na siyo wa
kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali sahihi ambapo shughuli
hizo zinaweza kufanywa.
Amesema mbali na shughuli za
madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika sekta za kilimo, maji na
ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua aina ya udongo unaofaa
kwa shughuli hizo.
Kutokana na umuhimu wa utafiti
na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu Waziri Biteko ametoa
wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika shughuli za kitaalam
ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta ya madini na kuongeza
kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake.Aidha,
Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China
kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo
ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Jilojia ya China, Profesa Sun Xiaoming amesema kuwa
taarifa ya utafiti iliyowasilishwa ni ya nchi nzima ya Tanzania na eneo
la Mkoa wa Mbeya.Amesema utafiti huo umetoa matokeo ya jiokemia ya
sampuli 71 nchini kote na sampuli 39 katika mkoa wa Mbeya na kuongeza
kuwa utafiti huo utasaidia katika utekelezaji maendeleo ya shughuli za
madini, kilimo na mazingira nchini.
Awali, akizungumza katika kikao
hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mathias Abisai amesema
kusudio la ujumbe huo ilikuwa ni kuhakiki kazi iliyofanyika na
kuwasilisha ripoti. Ameongeza kuwa, ripoti hiyo itasaidia kwenye tafiti
nyingine za madini ikiwemo maji na mazingira.
Ameongeza kuwa, mnamo Mwaka 2009
serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Jiolojia
zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huo wa
miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013 na
kukamilishwa mwaka 2018.
Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa
GST, Yokobeth Myumbilwa akileza malengo ya utafiti huo amesema kuwa ni
kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata
ambayo itaainisha uwepo wa taarifa zinazo ainisha uwepo wa aina
mbalimbali za madini ,upangaji miji ,pamoja na taarifa hizo kuweza
kutumika katika shughuli mbalimbali katika sekta za kilimo na mazingira.
No comments :
Post a Comment