Angel Msangi akizungumza jambo na waadishi wa habari leo katika Taasisi ya Mifupa MOI, Dar es Salaam. wa pili kulia ni Askari wa jeshi la Polisi CCP Moshi, Julius Msangi ambaye ni mume wa Angel Msangi na wa kwanza kushoto ni Dkt, Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani |
Dkt,
Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na
Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akimuelekeza Angel Msangi
kufanya mazoezi ili ajiridhishe mgonjwa wake wakwanza aliye fanyiwa
upasuaji wa kuondoa uvimbe katika mishipa ya ubongo kujiridhisha kama
amepata nafuu apate kumpa ruhusa ambapo upasuaji huo ulichukua muda wa
saa 6. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSS)
Dkt, Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehem ndogo iliyotumika kuondoa uvimbe huo
Dkt,
Bingwa wa Upasuaji wa Taasisi ya Mishipa ya Ubongo, Uti wa Mgongo na
Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Hamisi Shabani akizungumza jambo na
waandishi wa habari (hawapo pichani)
NA KHAMISI MUSSA
Taasisi
ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imefanikiwa kufanya upasuaji kwa mara
ya kwanza hapa nchini kuondoa vivimbe katika mishipa ya damu ya ubongo
(Aneurysm) ya mgonjwa.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Alhaji Dkt.
Hamisi Shabani.(pichani) amesema kwamba kabla ya hapo wagonjwa walikuwa
wanafanyiwa upasuaji huo nje ya nchi kwa gharama kubwa isiyopungua
shilingi za kitanzania milioni 100.
Akiongea
na waandishi wa habari, Dkt.Shabani amesema kwamba aina hii ya upasuaji
unahitaji darubini na vifaa tiba maalum ili kufanikisha upasuaji huo.
"Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutupatia vifaa vyote
ambavyo ni muhimu ili kufanikisha upasuaji huu.
Na
kuanzia sasa wagonjwa kama hao hawatapelekwa tena nje ya nchi
watafanyiwa hapa nchini kwa gharama nafuu isiyozidi shilingi milioni
10".
Naye
Angel Msangi (37) ambaye ni mgonjwa wa kwanza kufanyiwa aina hii ya
upasuaji alisema kwamba anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kuwa mgonjwa wa
kwanza kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo kwa mafanikio kwani asingemudu
gharama za upasuaji nje ya nchi.
"Pia
nawashukuru Madaktari wa Taasisi ya Mifupa MOI kwa kuniwezesha
kunifanyia upasuaji huu na kuwashukuru wauguzi wa Taasisi hii kunifanyia
upasuaji huu na sasa nina uhakika wa kuishi kwani nilikuwa nasumbuliwa
na tatizo la kupoteza kumbukumbu na nikiweka kitu nakuwa sijui
nimekiweka wapi, nikiwa nimekula nasahau kama nimekula, kwa hiyo kwangu
ikawa ni shida tayari".
Aidha
Dkt. Shabani alisema kwamba aina hii ya vivimbe huwapata watu wengi
lakini sio rahisi kugundulika kama una tatizo bila kufanya kipimo maalum
cha CT-Scan. " Asilimia 5 ya watua wazima wenye umri kuanzia miaka 30
ndio waathirika wakubwa.
Nchini
Marekani wamefanya utafiti na kugundua kwamba asilimia 5 ya watu wazima
wanaathirika na matatizo haya.Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)
zinaonyesha kwamba kwa kila watu 100 watu 10 wanakabiliwa na tatizo
hili". Alisema Dkt Shabani.
Athari za vivimbe vya damu kwenye ubongo ni pamoja na kupooza na kupoteza fahamu na kumbukumbu kwa mgonjwa.
No comments :
Post a Comment