Daktari
bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George
Longopa katika picha ya pamoja na beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar
baada ya kuwasili katika taasisi hiyo akiwa na daktari wa timu ya Simba Yassin
Gembe kufanyiwa vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiliwa na klabu hiyo
kupitia dirisha dogo jana Jijini Dar es Salaam.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George
Longopa akimfanyia beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar kipimo cha
kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipowasili katika
taasisi hiyo kufanyiwa vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiriwa na klabu ya
Simba jana Jijini Dar es Salaam.
Fundi
Sanifu wa Moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Saada Salum akimwekea kifaa cha kupima kiwango cha afya ya moyo ili kuhimili
mchezo awapo uwanjani beki wa Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar kabla ya
kusajiriwa na klabu ya Simba jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Daktari
bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa
akiangalia mapigo ya moyo na umeme wa moyo unavyofanya kazi katika mashine ya Trade Mill alipokua akimpima beki wa
Ivory Coast Coulibaly Zana Oumar vipimo vya afya ya moyo kabla ya kusajiriwa na
klabu ya Simba jana katika Taasisi hiyo.
No comments :
Post a Comment