Thursday, November 1, 2018

EALA YAPITISHA MUSWADA WA TAKWIMU


dsc_0516
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Bunge la Afrika mashairiki (EALA)jana limepitisha Muswada wa sheria ya
Takwimu ambapo muswada huo ni muhimu sana wakati jumuiya hiyo
inaelekea kwenye sarafu ya pamoja.
Akichangia katika bunge hilo Mbunge wa Afrika Mhandishi Mohammed
Habibu Mnyaa amesema kuwa muswada huo umekuwa umerudiwa rudiwa 
sana
na hivyo kuchukuwa muda mrefu hadi kupitiswa kwake.
Amesema kuwa kuchukuwa muda mrefu ilikuwa ni kutaka baadhi ya tafsiri
zirekebishwe hususani zilizokuwa zinailenga Nchi ya Tanzania ikiwemo
ya wakuu wa bodi za takwimu kuwa wajumbe katika kamati.
Jambo hilo lilipelekea kupigana hadi kuhakikisha kuwa muswada huo
unapitisha wajumbe huru kuingia katika kamati na wakuu hao kuwa huru
kama wajumbe ili kuepusha nchi kuleta takwimu zenye maslahi na taifa
lao.
“Muswada huu utasaidia sana wakati nchi za jumuiya zikielekea kwenye
sarafu moja ambapo nchi wanachama zitaleta wajumbe huru ambao wataleta
takwimu sahihi zitakazosaidia nchi yetu na jumuiya kulinda
maslahi”alisema Mhandisi Mnyaa.
Amsema kuwa kila wakati muswada huo ulikuwa unarudiwa kwa sababu
tulitaka baadhi ya tafsiri zirekebishwe hususani zilizokuwa zinailenga
nchi ya Tanzania hivyo kupitishwa italeta faida kwa jumiya yetu.
Kupitisha muswada huo na kupitisha kufingu kinachopinga wakuu wa
takwimu wan chi wanachama kuwasilisha muswada wa takwimu kwa kamati
itakuwa ni kuleta takwimu zinazoleta unafuu kwa nchi zao

No comments :

Post a Comment