Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Damas Ndumbaro (Mb.) akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Maiasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla kuongea na
waandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo.
Viongozi hao walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kuelezea
mikakati inayochukuliw na Serikali ya awamu ya tano ya kuvutia utalii
nchini. Mikakati hiyo imeanza kuzaa matunda ambapo wnanchi wa Urusi
wameichagua Tanzania kuwa eneo bora zaidi kwa utalii duniani na kutoa
Tuzo maalum kwa serikali. Aidha, Mikakati iliyofanywa nchini China hivi
karibuni imewezesha kuingiwa kwa Mkataba wa kuleta watalii elf 10 kutoka
Shangai mwaka 2019. Kushoto ni Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri popov. |
No comments :
Post a Comment