Katibu
mkuu wizara ya Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkt John
Jingu, akifanya zoezi la kutoa vyeti kwa wahitimu mbalimbali wa chuo
cha Ustawi wa Jamii leo Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu
wa chuo cha Ustawi wa jamii waliotunukiwa tuzo ya uzamili na Dkt John
Jingu wakati wa mahafali hayo leo Jijini Dar es Salaam
Wahitimu
wa shahada mbali mbali wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakila kiapo wakati
wa shughuli ya mahafali hayo mbele ya Mgeni Rasmi Katibu mkuu Wizara ya
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu leo
Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wahitimu wa shahada mbali mbali katika sherehe za mahafali ya 42 ya chuo cha Ustawi wa Jamii leo Jijini Dar es Salaam
………………………………………………………………………………..
TAASISI
ya ustawi wa jamii (SOCIAL WORK) imewatunuku vyeti wahitimu 1387 katika
mahafali ya (42) ya chuo hicho katika ngazi ya astashahada,stashahada,
katika fani ya Kazi za jamii kwa Watoto na vijana,Mahusiano kazini na
Menejimenti ya sekta ya Umma( industrial Relations and Public
Management).
Akizungumzana na wanahabari jijini Dar es salaam katika mahafali hayo
Katibu Mkuu
idara kuu ya Maendeleo ya Jamii -Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Dr.John Jingu amesema kuwa wahitimu wote wamekula
kiapo kwa ajili ya kutumikia Taifa na ujuzi waliopatiwa ni rasilimali
kwa ajili ya ujenzi wa Taifa kwa ujumla.
“Fani
ya ustawi wa jamii( SOCIAL WORK) ni fani nyeti na muhimu katika jamii
na wanapaswa kuwa katika sekta mbalimbali kwani wahitimu hawa
wamefundishwa kujiajiri na kuajiri watu katika kaza”amesema Dkt Jingu.
Jingu
ameongezea kuwa “alikadhalika katika nchi zilizoendelea kuna hitajika
kuwa na mahafisa wa ustawi wa jamii na chuo kwa sasa kinatakiwa kuweka
wigo mpana kwa ajili ya kuendelea kuzalisha wataalam kwa lengo la
kusaidia jamii na manufaa ya nchi kwa ujumla”
Akizungumza
na wanahabari Kaimu Mkuu wa Taasisi, Mipango,fedha na utawala wa
Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Saliel Kanza, ameeleza kuwa taasisi hiyo
ina changamoto katika kutekeleza majukumu yake makuu matatu ambayo ni
mafunzo,utafiti na kutoa ushauri wa weledi.
“Changamoto
hizo ni upungufu wa vifaa vya Tehama katika kufundishia na kujifunza,
uchakavu na upungufu wa Miundombinu ya kujifunza na kufundishia ikiwemo
ofisi za walimu,vyumba vya semina,vyumba vya mihadhara(lecture theatre)
na zahanati”amesema Kanza.
Pia
Kanza amesema pamoja na ufinyu wa Mapato,Taasisi imeendelea kuweka
mikakati mbalimbali yakuboresha mazingira bora ya kusomea kwa
kubadilisha Matumizi kwa baadhi ya Majengo na kuwa vyumba vya mihadhara.
Aidha
amesema ununuzi wa samani za ofisini na kompyuta ili ziweze kusaidia
Wanafunzi na wahadhiri katika kujifunza na kufundishia,Kufanya ukarabati
wa Miundombinu ya Taasisi kama vile vyumba vya mihadhara kulingana na
uwezo wa kifedha uliopo.
Hata hivyo,mbali na kufanya hayo bado Taasisi Haina uwezo wa kutosha kifedha ili kutatua changamoto tajwa.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ,Bi Sophia Simba amewapongeza
wahitimu hao na kuwataka watumie elimu yao na ujuzi ili kusaidia jamii
katika usuluhishi wa Migogoro mbalimbali katika jamii zetu.
Simba
amewahusia wahitimu katika fani zote kuwa ni kila nyanja katika jamii
inauhitaji wa Afisa ustawi kwani ni watu wenye ufanisi mkubwa sana
katika kutatua matatizo ya jamii,kusuluhisha,kusaidia maeneo yote kwa
walemavu,makazini hata Mashuleni.
“wataalam
hao ni matumaini ya nchi kuwa watatumiwa vema na Serikali na wadau
katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya jamii” amesema Sophia Simba.
No comments :
Post a Comment