Thursday, November 1, 2018

DKT. DAMAS NDUMBARO AAPISHWA BUNGE LA EALA


708A8541
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Naibu waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Damas Ndumbaro amesema kuwa Atahakikisha analinda maslahi ya Tanzania
katika Bunge la Afrika Mashariki sanjari na kushirikiana na wenzake
kutatua changamoto za jumuiya hiyo.
Dkt.Ndumbaro ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa katika bunge la

Afrika mashariki (EALA) ambapo akatolea mfano changamoto ya  sheria
takwimu jinsi ilivyochukuwa muda hadi jana kupitishwa na bunge hilo.
Amesema kuwa atahakikisha analinda maslahi ya nchi katika jumuiya ya
Afrika mashairiki na kutoa wito kwa ngazi zote kuhakikisha
wanafanyakazi pamoja na maamuzi pamoja lengo ni kutatua changamoto
zinazoikabili jumuiya hiyo kwa manufaa yaTanzania na jumuiya hiyo kwa
ujumla.
“Kuanzia wabunge sekretariet ya jumuiya baraza la mawaziri na wakuu wa
nchi wananchama kufanyakazi kwa pamoja lengo likiwa ni kuongeza
mtangamano katika jumuiya hiyo”alisisitiza Dkt Ndumbaro.
Amesema kuwa anamshukuru sana Dkt.John Magufuli kwa kumteua kuwa naibu
waziri katika kumsaidia majukumu yake ambapo ntahakikisha anachapakazi
kwa kulinda maslahi ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla.
Amesema kuwa jumuiya yoyote haikosi changamoto hata jumuiya ya Ulaya
inakabiliwa na changamoto ndio maana hata uingereza ikaamua kujitoa
hivyo hivyo hata jumuiya yetu ina changamoto mbali mbali kikubwa ni
kuzikabili kwa pamoja kuhakikisha jumuiya inadumisha matangamano.
“Najua jumuiya inapitia kwenye changamoto mbali mbali hata umoja wa
mataifa una changamoto zake,vile vile umoja wa ulaya una changamoto
zake hata uingereza wamejitoa hizo ni changamoto mfano changamoto ya
muswada wa sheria ya Takwimu umechukuwa muda mrefu hadi leo ndio
unapitishwa”alisema Ndurmbaro.

No comments :

Post a Comment