Thursday, November 1, 2018

TIC yazitaka Taasisi zote kuvutia mazingira ya uwekezaji


th
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geoffrey Mwambe amezitaka Taasisi na Mashirika ya Serikali kutathmini mifumo yao ya utendaji kazi na kuangalia maeneo muhimu ya kuyafanyia kazi ili kuharakisha juhudi za kuvutia wawekezaji Nchini.
Mwambe amesema Kila Sekta na Taasisi Nchini zinayo maeneo muhimu ya kuvutia wawekezaji na hivyo juhudi za dhati zinahitajika katika kuimarisha maeneo hayo ambayo
yataimarisha uchumi wa Taifa.
“Kila Wizara, kila Idara,kila Taasisi ya Serikali itambue inahitaji kufanya nini ili kuweza kuvutia uwekezaji, kila Sekta ijitathmini inafanya nini katika kurekebisha mfumo wao ili kuvutia wawekezaji, watu wengi wanadhani suala la nuwekezaji ni la Wizara ya Viwanda na Biashara tu,wengine wanadhani ni suala la Kituo cha uwekezaji tu,hapana ni la kila Wizara na la kila mtu hivyo ni lazima sekta zote zifanye juhudi za kuvutia uwekezaji” Alisema Geoffrey Mwambe Mkurugenzi Mkuu wa TIC.
Mwambe amesema Kituo chake kimefanya jitihada nyingi za kuhamasisha wawekezaji ambao wanakuja kuwekeza nchini hivyo hatua za baadhi ya watendaji wa Serikali za kukwamisha juhudi hizi hazikubaliki
“Jamani huko Duniani tunanyang’anyana wawekezaji, hata nchi zilizoendelea zinahamasisha wawekezaji waende kuwekeza kwao,sisi hapa kwetu tunahamasisha waje na wakija kuna baadhi ya watendaji wa Serikali wanawakwaza,hili halikubaliki” alisema Geoffery Mwambe Mkurugenzi Mtendaji wa TIC.
“huko nje tunakotafuta soko ni moja,nchi nyingi zinavutia wawekezaji hata zile zilizoendelea hivyo tunagombania wawekezaji,tunatumia nguvu kubwa ya kuhakikisha tunapata wawekezaji tunaitangaza nchi yetu kuhusu vivutio vya uwekezaji” alisemaMwambe.
Amesema atawataja na atapeleka Majina yao kwa Rais Magufuli wale wote wanaokwamisha juhudi hizi za Serikali za kuhamasisha uwekezaji ambao unalenga kuimarisha uchumi wa Taifa na kuifanya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati.
Mwambe alikuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumzia mafanikio ya safari yake ya Geneva Nchini Uswis kuhudhuria kongamano kubwa la uwekezaji lililofanyika Oktoba 2 hadi 26 mwaka huu lililohusisha wakuu wanchi na Viongozi wakuu wa taasisi za uwekezaji lililoandaliwa na Shirika la umoja wa mataifa la maendeleo ya Biashara la UNCTAD ambao ulihudhuriwa na Marais 11 pamoja na Mawaziri 53 Duniani.
Amesema Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya biashara UNCTAD kwenye kongamano hilo wametoa mwenendo wa uwekezaji kwenye Nchi mbalimbali Duniani ambapo kwa mwaka 2016 kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji kwa kupata uwekezaji wa shilingi Bilioni 1.565 ikifuatiwa kwa mbali na Nchi ya Uganda kwa Shilingi milioni 580

No comments :

Post a Comment