*Awe ameshatoa fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu
WAZIRI MKUU Kassim ametoa siku
10 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Bw. Peter Swea
awe ametoa fedha za mikopo kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu.
“Leo ni tarahe 10 nataka hadi
ikifika tarehe 20 ya mwezi huu uwe umeshatoa fedha za mikopo kwa
wanawake, vijana na walemavu. Habari za mpaka kikao kiridhie hayo ni
mambo ya
zamani na ndio maana ikatungwa sheria kwa ajili ya jambo hilo. “
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo
leo (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kata
ya Kibakwe wilayani Mpwapwa mara baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha
Afya cha Kibakwe, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo
baada ya Mkurugenzi huyo kumueleza kuwa bado hajatoa fedha kwa ajili ya
mikopo hiyo ambazo alipaswa kuzitoa kila robo mwaka, akidai bado kikao
cha kuidhinisha hakijakaa.
Amesema fedha hizo ambazo ni
asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayokusanywa kwenye halmashauri, ambapo
anatakiwa kutumia asilimia nne kwa ajili ya mikopo ya wanawake,
asilimia mikopo kwa ajili ya vijana na asilimia mbili zitolewe kwa
walemavu.
Kadhalika,Waziri Mkuu
amewaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye misitu
na vyanzo vya maji pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wote
watakaobainika kukata miti bila kibali.
Amesema mtu yeyote
atakayebainika kukata miti bila kibali achukuliwe hatua kali kwa sababu
wamekuwa wakisababisha ukosefu wa maji, ambapo wakandarasi wa maji
kwenye wilaya hiyo wanapata changamoto ya kukosa maji kwenye maeneo
mengo wakati awali Mpwapwa awali ilikuwa na ardhi ya chepechepe.
“Nimepata habari, hapa Kibakwe
watu wanakata miti ili kushindana ubavu wao wa kuishi. Nawaagiza
watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yenye vyanzo vya maji na
misitu na muyalinde. Madiwani pia mnatakiwa kushiriki kukemea ukataji
miti.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya
Mpwapwa, Bw. Jabir Shekimweli ameishukuru Serikali kwa kutenga sh.
bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vitatu vya afya
ambavyo ni Kibakwe, Mima na Pwaga.
Amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na kamati za ujenzi kwenye kata na vijiji husika kama ambavyo muongozo ulivyoelekeza.
NayeMbunge wa Jimbo la
Kibakwe, Bw. George Simbachawene amesema utekelezaji wa Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) umefanyika kwa mafanikio makubwa kwenye sekta ya
afya, umeme na elimu.
Mbunge huyo ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, ameomba ujenzi wa barabara ya
kiwango cha lami kutoka Kongwa, Mpwapwa hadi Kibakwe, uharakishwe ili
kuondoa adha ya miundombinu inayowakabili wananchi.
No comments :
Post a Comment