Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) akizungumza na Mtendaji
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka(kushoto) mara
baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika chuo ambapo alizungumza
na watumishi wa chuo hicho katika Kampasi ya Temeke, jijini Dar es
Salaam.
- aibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(wa pili kushoto) akizungumza na watumishi wa chuo hicho katika Kampasi ya Bustanini , jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akiwa na Mtendaji
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka wakiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chuo mara katika Kampasi ya
Bustanini jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) akizungumza na Mtendaji
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Sedoyeka(kushoto) mara
baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika chuo ambapo alizungumza
na watumishi wa chuo hicho katika Kampasi ya Temeke, jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) akiwa ameongoza na
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo
Sedoyeka(kushoto) mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika
chuo hicho katika Kampasi ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga(katikati) akipewa maelezo na
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo
Sedoyeka(kushoto) kuhusiana na vyumba vipya vya kulala wageni
vilianzishwa katika chuo hicho mara baada ya Naibu Waziri huyo kufanya
ziara katika chuo hicho katika Kampasi ya Bustanini jijini Dar es
Salaam.
- Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akinagalia baadhi ya majiko ambayo yamekuwa yakitumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii wakati wa mafunzo kwa vitendo.
……………………….
Serikali imekiagiza
Chuo cha Taifa cha Utalii ifikapo Januari mwakani kianze kutoa usajili
na utambulisho kwa watu wanaotoa huduma kwa watalii.
Usajili huo unapaswa
kwenda sambamba na mitihani watakayofanya walengwa kuhakikisha kama
wamebobea kutoa huduma hizo kwa watalii.
Agizo hilo limetolewa
leo na Mhe.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
alipokutana na watumishi wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mhe.Hasunga
ameelekeza watu wote wanaohusika kuhudumia watalii kufanya mitihani hiyo
ya kuhakikiwa ili kutambulika na kupata usajili kwa hiari baada ya hapo
wasiosajiliwa hawataruhusiwa kufanya kazi hizo.
Amesema lengo la usajili huo ni kulinda fani ya huduma za utalii na ukarimu inayoonekana kuvamiwa na watu wasiokuwa na sifa.
“Mtalii hawezi kurudi nchini kama amehudumiwa na watu wasiokuwa na ukarimu na sifa zisizofaa,
“Ukipita kwenye
hoteli huko unakutana na vitu ambavyo havivutii kabisa kwa sababu kuna
wavamizi wamevamia, sasa hilo lifike mwisho nataka kuanzia Januari wote
watambulike,”
Mhe.Hasunga pia
ameagiza wakufunzi wa chuo hicho kufanya tafiti na kuandika machapisho
ya kitaaluma kwenye eneo la utalii na maliasili.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Dk Shogo Sedoyeka changamoto kubwa
waliyonayo ni kupata eneo kwa ajili ya kampasi ya Temeke.
Amesema,” Lile eneo
tunatakiwa kuhama kwahiyo tunahangaikia kupata ardhi ili tuhamishe
kampasi na itakuwa huru kwetu kwa sababu litakuwa eneo letu,”.
No comments :
Post a Comment