MTWARA
Na,Omary Hussein.
Naibu waziri wa Viwanda,Biashara
na Uwekezaji Stella Manyanya amewataka wawekezaji walioshindwa
kuendeleza maeneo yao kwa muda mrefu, hususani wamiliki wa viwanda
vilivyo binafsishwa, kutumia busara kwa kueleza ukweli ili serikali
ichukue hatua ya kuviwezesha viwanda hivyo kufanya kazi.
Naibu waziri ameyasema hayo Mkoani
Mtwara akiwa katika kiwanda cha kutengeneza Cement cha Dangote, baada
ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja, iliyolenga kujiridhisha na hali
ya viwanda mkoanihumo.
‘Sisi kama serikali tusingependa
kuona wawekezaji wakashindwa kujiendeleza bila sisi kuwasaidi lakini ni
kwawale tu wenye nia ya dhati ya kuwekeza,niwahakikishie tu wawekezaji
Tanzania ukiwemo mkoa huu wa mtwara nisehemu salama kwa wawekezaji wenye
nia, nasisi tutakua nao bega wa bega’ alisema Naibu waziri Manyanya.
“Ila kwa wale ambao wanataka
kujaribu kutuchezea wnasema wanawekeza lakini hawana nia ya kuwekeza
pengine wanatafuta tu fursa za kushika soko ili waonekane wamezuia
halafu wanawekeza maeneo mengine kwakweli hao hatutawavumulia” Aliongeza
Naibu waziri Manyanya.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Mtwara Evod Mmanda ameshukuru ujio wa Naibu waziri huyo akisema
wanapokuja viongozi wa juu inasaidi kuweka hamasha kwa wawekezaji
wakiona serikali yao ipo pamojanao na inawaunga mkono kwa vitendo.
“Ujio wa naibu waziri katika
wilaya ya Mtwara sio wakazi wa Mtwara pekeyao wanao nufaika bali
inasaidia hata kwa wawekezaji wanaoendesha viwanda pamoja na wafanyakazi
kuona serikali inawajali”.Alisema mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda.
No comments :
Post a Comment