Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akionesha Ripoti
ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi
Tanzania mara baada ya kuizindua, kushoto ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
NA
MUNIR SHEMWETA, DODOMA
NAIBU Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kasi ya utoaji hati za
umiliki wa ardhi na makazi imeongezeka kwa kasi ambapo hadi kufikia septemba
mwaka huu 2018 jumla ya hati 25,463 zimeandaliwa. Akizungumza
wakati wa kufungua mkutano wa uwasilishwaji matokeo ya utafiti kuhusu haki na
usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi jijini Dar es salaam leo Mabula
alisema jumla ya hati 17,680 zilikuwa zimewasilishwa ofisi za kanda kwa ajili
ya usajili na hati 9,739 zimeshakamilika. Hata
hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema pamoja na
jitihada zinazofanywa na Wizara yake katika kutoa hati lakini takwimu zinaonesha
kuwa hati nyingine zimeandaliwa katika halmashauri lakini zilizowasilishwa
kwenye ofisi za kanda husika ni chache kutokana
na kukosekana kwa vifaa vya kuandalia hati. Kwa
mujibu wa Mabula, kuna hati nyingi zinaonekana kuwasilishwa ofisi za kanda lakini
hati zilizokamilika ni chache kutokana na hati nyingi zilizowasilishwa katika
ofisi za kanda kuwa na upungufu mbalimbali na hivyo kusababisha hati hizo
kutokamilika kwa wakati. Akigeukia
suala la haki na usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi kwa wananchi
waishio vijijini, Mabula alisema hadi kufikia Mei 2018 jumla ya vipande vya
ardhi 96,257 vimepimwa katika vijiji 91 na hati za kimila 20,583 zimeandaliwa
na vijiji 20 vimeandaliwa na mipango ya makazi ambapo jumla ya viwanja 18,224
vimepimwa kwa ajili ya kuandaliwa hati ya haki miliki ya kimila. Kwa
mwaka 2018/2019 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga
kuandaa hati za kimila 120,000, mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji
30 na mpango wa kina kupima viwanja 20,000 kwa lengo kumuwezesha mwananchi wa
kawaida kuwa na uhakika na usalama ya miliki yake na kuepusha migogoro.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Angelina Mabula akimkabidhi Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Frank
Mvungi Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi
na Makazi Tanzania
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Angelina Mabula akimkabidhi Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa
Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda
ya Kati Ezekiel Kitilya mara baada ya kuizindua ripoti hiyo.
No comments :
Post a Comment