Monday, October 1, 2018

HAKIKISHENI WAFANYAKAZI WANAELEWA WAJIBU NA HAKI ZAO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI-SSRA


 Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kushoto), akimpongeza mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Tathmini, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA), Bw. Joseph Mutashubilwa, baada ya kufungua magfunzo ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyowaleta pamoja viongozi na watendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) na kufanyika mjini Morogoro Oktoba 1, 2018.
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi.
Bw.Mutashubilwa, (aliyesimama) akitoa hotuba hiyo. Kushoto ni Bw. Anselim Peter na kulia ni Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw.Henry Mkunda
NA K-VIS BLOG, MOROGORO
 Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, akizunguzma kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter akitoa mada.

Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Hery Mkunda, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
 
 Bw. Peter (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada.
 Mshiriki kutoka TUGHE Kilimanjaro, Simon E Msuya, akizungumza
  Mshiriki kutoka mkoa wa Morogoro, …..akizungumza
 Katibu Mkuu wa TUGHE, Bw. Hery akiuliza swali kuhusu utaratibu wa kutoa mafao kwa mtu aliyepata ajali wakati akitekeleza majukumu ya kazi ya mwajiri
 Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE taifa (Afya) Mhandisi Amani Msuya akizunhgumza
 Mwakilishi toka Mkoa wa Tanga, Bi. Flora C Urassa akiuliza swali.
 Mwakilishi toka Mkoa wa Mbeya, Bi.Janeth Masawe, akiulzia swali.
 Bw. Rugemalira M. Rutatina, akiuuliza swali.
 Mwakilishi toka Mkoa wa Pwani, Bw. Shadrack C. Mkodo akiuliza swali.
 Mwakilishi wa TUGHE Mkoa wa Ruvuma Bw. Athanas B. Tarimo akiuliza swali.
Bw. Steven R. Wadi akiuliza swali, (kulia) ni Msimamizi na mjuongozaji wa semina Bi. Laura Kunenge.

Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Anselim Peter, (kushoto), akibadilishana mawazo na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Bw. Mchenya M. John
Meneja wa huduma za Sheria Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Kitandu Ugula (kushoto), akibadilishana mawazo na Afisa Uhusiano na Uhamasishaji Mamlaka hiyo, Bi. Zawadi Msalla
 Meza kuu katika picha ya pamoja kundi la kwanza
  Meza kuu katika picha ya pamoja kundi la pili.
  Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi.
Bw.Mutashubilwa, (aliyesimama) akitoa hotuba hiyo. Kushoto ni Bw. Anselim Peter na kulia ni Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw.Henry Mkunda
NA K-VIS BLOG, MOROGORO
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA) Dkt. Irene Isaka, amewataka viongozi na watendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) kuhakikisha wanachama wao wanafahamu wajibu na haki zao katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Dkt. Isaka ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa viongozi na watendaji wa TUGHE taifa na mikoani  iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Utafiti na Tathmini SSRA, Joseph Mutashubilwa mjini Morogoro Jumatatu Oktoba 1, 2018. “Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaepusha migogoro na tunadumisha mahusiano sehemu za kazi hali itakayowavutia wawekezaji kuja nchini kwa wingi na hivyo kutimiza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.” Alsiema Dkt. Isaka. Dkt. Isaka pia aemwataka washiriki hao wa mafunzo kusambaza elimu watakayoipata kwa kuwatembelea na kuwapa elimu wanachama wa chama hicho na kumtaka kila kiongozi/mtendaji aliyeshiriki awe na mpango kazi utakaoonesha idadi ya wanachama alionao katika eneo lake na namna atakavyowafikishia elimu hii ambayo ni muhimu kwao kuifahamu.“Nina imani kwa kufanya hivi tutakuwa tumewasaidia kwa kiasi kikubwa wanachama wetu kuujua Mfuko, kazi zake na pia kufahamu nini wanapaswa kufanya baada ya kupata matatizo wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri.” Alifafanua. Akinukuu kifungu cha 72 (4) cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, Mkurugenzi Mkuu huyo wa SSRA alisema kifungu hicho chan sheria kinatamka nafasi ya uwakilishi wa vyama katika kamati za afya na usalama mahali pa kazi ambapo mwajiri anatakiwa kutunza kumbukumbu hizo na kamati inatakiwa kukagua ili kuona kama hilo linafanyika. Hayo yote ni katika kuhakikisha kwamba upo ushirikishwaji wa baina viongozi/watendaji na Serikali katika kulinda afya za wafanyakazi sehemu za kazi. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter alisema, semina hiyo ya mafunzo ni muendelezo wa hatua ya Mfuko kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ambayo ni wadau wa Mfuko na nia kubwa ni kuwajengea uelewa wa madhumuni ya kuanzishwa kwa Mfuko, Sheria na jinsi Mfuko unavyofanya kazi. Alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu yake, kumekuwepo na mafanikio makubwa ya kutimiza jukumu kuu la kuanzishwa kwa Mfuko la kupokea madai na kulipa fidia na hadi sasa Mfuko tayari umekwishalipa fidia zaidi ya shilingi bilioni 4.4. Naye Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw. Hery Mkunda, yeye alisema, mafunzo hayo yatawezesha kuongeza uelewa kuhusu wajibu wa mwajiri na haki kwa mfanyakazi katika kuelewa sheria hiyo ya Fidia. “Washiriki hawa ambao ni Makatibu wa Mikoa wa TUGHE ambao wao ndio husimamia haki na maslahi ya wafanyakazi sehemu zao za kazi kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao kwa mujibu wa sharia watakuwa mabalozi wazuri katika kufikisha elimu hii kwa wanachama wetu.” Alisema.
Alisema kadisi siku zinavyokwenda, uelewa kuhusu shughuli za Mfuko umekuwa ukikua na kwamba hii imekuwa fursa nzuri kwa watendaji wa TUGHE ili waendelee kufuatilia na kuwafundisha wanachama wetu kuhusu haki zao hususan katika masuala haya ya Fidia kwa wafanyakazi.
Alisema TUGHE kwa sasa ina jumla ya wanachama 70,000 na lengo la chama ni kuongeza wanachama 10,000 kila mwaka kwa picha hiyo TUGHE ni "jeshi" kubwa na washiriki wa mafunzo ni makatibu wa mikoa ambao ndio wanashughulika moja kwa moja na wanachama kwa hivyo elimu itafika kwa walengwa.
"Matokeo ya semina hii ni hoja zilizojengwa na uongozi wa TUGHE tawi la WCF kwenye kkkao cha baraza la wafanyakazi kuonyesha umuhimu wa elimu hususan watendaji wanaoshughulika moja kwa moja kuwa na uelewa kuhusiana na shughuli za Mfuko.
"Tunawashukuru sana WCF kwa kuwezesha mafunzo haya na kimsingi watendajin wote kutoka TUGHE makao makuu na makatibu wa mikoa wamehudhuria." Alisema Bw.Mkunda.

No comments :

Post a Comment