Monday, October 1, 2018

PROFESANDALICHAKO AWATUMBUA MKURUGENZI WA MAFUNZO YA UALIMU NA MRATIBU WA MIRADI WA WIZARA YA ELIMU

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na viongozi wengine wakiangalia mashimbo ya msingi ya ujenzi wa majengo mbalimbali ya upanuzi wa Chuo cha Ualimu Ndala jana akiwa kwenye ziara Mkoani Tabora. Kazi hiyo ambayo haikumridhisha Waziri imefanyika kwa muda wa miezi sita.
Skauti wa Chuo cha  ualimu Ndala wakimwongoza Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kuelekea kwenye Ofisi za Utawala wakati wa ziara yake jana katika Chuo hicho.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia jana.

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akitoa tamko la kumuondoa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu na Mratibu wa Miradi wa Wizara hiyo jana baada ya kuonekana kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.

Mkuu wa Chuo cha Ualimu Ndala Abinego Ndikumwe akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati wa baadhi ya majengo na upanuzi wa Chuo kwa Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jana

Eneo la ujenzi wa mabweni, kumbi za mihadhara na majengo mengine kwa ajili ya upanuzi wa Chuo cha Ualimu Ndala kama linavyoonekana ikiwa ni kazi ya miezi sita chini ya Kampuni ya Skywards. Mradi huo ni wa bilioni 4.6 Serikali imeshamlipa milioni 600 na bado miezi 11 akabidhi majengo.


Wanachuo wa chou cha ualimu Ndala wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumpokea Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako(hayupo katika picha) wakati wa ziara yake jana katika Chuo hicho.

No comments :

Post a Comment