Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akipokea taarifa ya Elimu ya Mkoa wa Ruvuma
kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema wakati wa ziara
ya kukagua miradi ya Elimu Mkoi huko.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa mwalimu wa somo
la uchomeleaji (welding) Onesmo Pela katika Chuo cha Ufundi Veta Songea
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha
Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Namtumbo kilichopo katika Wilaya
ya Namtumbo Wilayani Ruvuma
………………………………
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki moja kwa mtaalamu Elekezi wa
Kampuni ya Archquants Service Limited kuhakikisha inawasilisha michoro
ya kazi za nje ya Chuo cha ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo
kilichopo Mkoani Ruvuma ili ujenzi wa chuo hicho uweze kukamilika.
Mheshimiwa Ole Nasha ametoa agizo
hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema
ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa
mradi huo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri
Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA
kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro
mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo
Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo.
Naibu Waziri amesema ukanda wa
Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi
hiyo kutasaidia wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma
na baadae kutekeleza kwa vitendo.
“Serikali inatilia mkazo Elimu ya
ufundi na imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi
kupata Elimu ya ufundi na ndio maana Serikali ya awamu ya Tano imeamua
kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza Naibu
Waziri Ole Nasha
Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani
Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya
Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia.
No comments :
Post a Comment