Imeelezwa
kuwa Taasisi ya kupambana na Rushwa mkoa wa Arusha imepokea jumla ya
malalamiko 108 kwa njia mbalimbali ikiwa ni jitihada za kupambana na
rushwa mkoani hapo.
Akitoa
ripoti ya miezi mitatu ya kiutendaji Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa
Arusha Frida Wikesi amesema taarifa hizo zimehusu halmashauri
mbalimbali katika mkoa, idara ya ardhi, Nida, afya, kilimo, elimu,
serikali za vijiji na mahakama
Amesema
jumla ya majalada 23 ya uchunguzi yalifunguliwa na yanaendelea
kuchunguzwa ambapo chunguzi hizo zipo katika hatua mbalimbali, haswa
zilizo katika muelekeo wa makosa ya rushwa.
Aidha
amesema sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 inashauri,
ushauri yakinifu kutolewa kwa watoa taarifa kwa malalamiko
yanayoonekana kutokuangukia kwenye sheria hiyo.
''
Malalamiko mengi yanayowasilishwa yanahusiana na rushwa, aidha kwa
kipindi tajwa jumla ya makosa mapya mawili (02)yamefikishwa mahakamani
'' alisema
Hata
hivyo amesema kuwa ofisi ya takukuru mkoa wa Arusha wamefanya dhibiti
moja la rushwa, na kuendesha zoezi la ufuatiliaji wa kuziba mianya ya
rushwa.
''
Hadi kufikia mwezi septemba 2018 jumla ya mashauri 18 yaliendelea
kusikilizwa mahakamani ambayo yalikuwa katika hatua mbalimbali za
mahakama"alisema Wikesi
Katika
kipindi tajwa TAKUKURU iliweza kuokoa jumla ya fedha kiasi cha
11,345,000 ambazo zililipwa kwa watumishi waliokua wakishughulikia
maonyesho ya 88 kanda ya kaskazini mwaka 2017(10,055,00) fedha
zilizokuwa za ujenzi wa mahabara sekondari ya Ilkiding'a Arumeru sh
1,290,000 ambazo zilirejeshwa serikalini.
No comments :
Post a Comment