Mdudu mbung’o
Firmi Banzi Mtaalamu wa masuala ya Nyuklia.Mdudu mbung’o
Dkt. Imna malele-mtaalamu wa magonjwa ya mifugo akizungumza na wanahabari baada ya ufunguzi wa mafunzo
NA VERO IGNATUS-ARUSHA.
JUMLA ya nchi 10 duniani
zimekutana jiji Arusha kwa lengo la kujifunza mbinu za kisasa na matumizi ya
tecknolojia,katika kudhibiti magonjwa ya mifugo yanayo ambukizwa na mdudu
mbung’o katika maeneo ya wafugaji na hifadhini.
Katika mazungumzo na wanahabari Mtaalam wa magonjwa ya mifugo Dkt
Imna Malele amesema kuwa mdudu mbung’o amekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji
wengi na baadhi ya maeneo ya hifadhi hivyo ni wakati muafaka kutumia mbinu za
kisasa katika kuangamiza mdudu huyo ambae amekuwa changamoto katika maeneo ya
wafugaji na hifadhini.
Amesema kwa nchi ya
Tanzania tatizo la kuwepo kwa magojwa yatokanayo na mdudu mbung’o bado ni
kubwa,na limekuwa likipunguza nguvu kazi katika uzalishaji kupitia mazao
yatokanayo na mifugo suala ambalo humnyima amani mfugaji endapo mifugo
itaathirika na magojwa yatokanayo na mbung’o.
Mara baada ya kufungua mafunzo hayo maalum kwa niaba ya mkurugenzi
mkuu wa tume ya nguvu za atomic nchini Prof Lazaro Busagala, Dkt. Firmi Banzi
ambae pia ni mtaalamu wa masuala ya teknolojia na masuala ya nguvu za nyuklia
akatumia fursa hiyo kueleza matumizi ya teknolojia ya nyuklia nchini
katika kupambana na mbung’o bila ya kuharibu mazingira ambapo amesema njia hiyo
imekuwa na manufaa makubwa katika nchi mbalimbali duniani.
Nao baadhi ya washiriki
akiwemo Deusdedit Malulu wakaeleza matarajio yao katika masuala ya utafiti
dhidi ya kuangamiza mdudu aina ya mbung’o kwa mazingira salama ya utalii ambapo
wamesema njia hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika jamii za wafugaji na
maeneo ya hifadhini.
Mdudu mbung’o hueneza
uonjwa wa malale ambao ni hatari kwa maisha ya binadamu ambapo pia njia ya
matumizi ya nyuklia imetajwa kuwa ni miongoni mwa njia salama katika mapambano
dhidi ya mbung’o ambapo njia hiyo imekuwa mkombozi zaidi katika visiwa vya
zanzibar na maeneo mbalimbali nchini.
No comments :
Post a Comment